Mdude Nyagali, Samehe! Nakupa pole mno kwa mambo yaliyokukuta

Mdude Nyagali, Samehe! Nakupa pole mno kwa mambo yaliyokukuta

MIGNON

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2009
Posts
4,108
Reaction score
5,110
Mdude_Nyagali

Kwanza nakupa pole mno kwa mambo yaliyokukuta. Umepitia mateso makubwa sana kwa sababu ya Imani yako ya kisiasa nakwa sababu ya uzungunguzaji wako na hoja zako.

Tangu ulivyotoka jela nimekusikiliza sana, kuanzia Clubhouse na kwingine kote ulipofanya mahojiano. Kwa kweli umeteseka!

Kuna wakati nilifuatilia sana mambo ya mateso katika vituo vya Polisi na kwa wafungwa mpaka wale wa Guatanamo; ukweli ni kuwa binadamu ni mgumu lakini pia binadamu ana roho ngumu.

Maisha yanaendelea, waliokutesa bado wapo, kama ni serikali bado ipo na kwa sababu hizo nakuomba usamehe na uendelee na Maisha yako ya kisiasa kwa mtizamo mpya. Yafukie mateso na jipange kwa kadri hali ya uwanja ilivyo.

Ni wengi wamepitia mateso kama yako lakini kwa kutaka amani ya kudumu wameamua kuyapa kisogo yaliyopita. Pole sana binafsi nitafurahi ukiwa una post picha ukiwa katika shughuli zako za kiuchumi au kisiasa. Ujumbe huu umfikie Tundu Lissu pia na wengine wote waliobahatika kupitia hayo na kutoka salama.

Uponye moyo wako.
 
Kabla hujamtendea mtu ubaya, kumbuka

Msamaha ni jambo la hiari.
 
Mdude yupo huru anaendelea na shughuli zake za ufundi wa radio na computer so amesha move on na kamsamehe The late Jpm na wafuasi wake wote .
 
Mdude yupo huru anaendelea na shughuli zake za ufundi wa radio na computer so amesha move on na kamsamehe The late Jpm na wafuasi wake wote .
Kam ni hivyo,hilo ni jambo la kushukuru.
 
MUDE NYAGALI

Kwanza nakupa pole mno kwa mambo yaliyokukuta .Umepitia mateso makubwa sana kwa sababu ya Imani yako ya kisiasa nakwa sababu ya uzungunguzaji wako na hoja zako.

Tangu ulivyotoka jela nimekusikiliza sana,kuanzia clubhouse na kwingine kote ulipofanya mahojiano.Kwa kweli umeteseka!!

Kuna wakati nilifuatilia sana mambo ya mateso katika vituo vya Polisi na kwa wafungwa mpaka wale wa Guatanamo;ukweli ni kuwa binadamu ni mgumu lakini pia binadamu ana roho ngumu.

Maisha yanaendelea,waliokutesa bado wapo,kama ni serikali bado ipo na kwa sababu hizo nakuomba usamehe na uendelee na Maisha yako ya kisiasa kwa mtizamo mpya.Yafukie mateso na jipange kwa kadri hali ya uwanja ilivyo.Ni wengi wamepitia mateso kama yako lakini kwa kutaka amani ya kudumu wameamua kuyapa kisogo yaliyopita.Pole sana binafsi nitafurahi ukiwa una post picha ukiwa katika shughuli zako za kiuchumi au kisiasa.Ujumbe huu umfikie Tundu Lissu pia na wengine wote waliobahatika kupitia hayo na kutoka salama.

Uponye moyo wako.
Naunga mkono hoja.
 
Acha aongee tu, uzuri wa mtu anayeongea inamsaidia ku process hayo magumu aliyopitia ambalo ni jambo zuri.

Hatari ni wale ambao wanatendewa ubaya alafu anaendelea tu na maisha yao kama hakuna kilichotokea vile, baada ya miaka kadhaa unasikia amechinja ukoo mzima wa adui yake.
 
Back
Top Bottom