Kwakifupi: Nikwamba ugonjwa ulianza mwaka 1991 nikiwa darasa la kwanza, Mguu ulianza kuniuma wenyewe baada ya hapo nikapelekwa hospilalini nikalazwa ukawa umevimba mguu wote vikatoka vidonda viwili vilikuwa vinatoa usaa na vipande vya mifupa. Mwaka 1993 ukaanza mkono ukatokea uvimbe baada ya muda ukapasuka na usaa na mifupa mingi ikatoka hadi mkono umelemaa nashindwa kuunyosha saiz tatizo limerudi tena mguuni unaniuma sana nimetumia dawa nyingi sipati nafuu napata maumivu makali sana dawa za kutuliza maumivu saiz hazifanyi kazi
Pole sana Vumilia. Kwani madaktari wanasema dawa hakuna kwa ugonjwa huo?? Kama hakuna basi jaribu za kienyeji kama ambavyo wenzangu wataendela kukupa ushauri. Mdalasini na Asali ni dawa pia ya magonjwa mengi. Pia umejaribu kufanyiwa maombi kwa imani unayo amini??? Naamini sana watumishi wa Mungu wale ambao si matapeli, wale wenye upako wanaombea na maajabu yanatokea. Hebu jaribu tena huko kulingana na imani yako inavyokutuma na uchaguzi wa mtumishi ambaye unaona anafaa.
Naamini pia Vumilia siyo jina lako halisi!!! Kama si halisi basi usipende kulitumia!!!! Majina mengine yana reflect hali halisi ya maisha ya baadaye, Imagine kumpa jina mtoto, Matatizo, Shida, Tabu, Vumilia, Maneno, Makelele, Mangumi, Makusaro, Tatizo, Vita, n.k!!! Majina mema yamebeba mema kwa watoto wako mf. Furaha, Sia, Zawadi, Rikiki, Baraka, Amani, Imani, Tumaini, Upendo, Pendo, Busara, etc.
Hata kama umepitia mabonde na milima katika maisha yako, usimpe mtoto jina linaloambatana na mateso au ambalo lina maana isiyo njema katika jamii. Ni mawazo yangu tu wakuu.