Uchaguzi 2020 Meatu CHADEMA: Uchukuaji wa fomu waenda vizuri

Uchaguzi 2020 Meatu CHADEMA: Uchukuaji wa fomu waenda vizuri

guwe_la_manga

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2019
Posts
2,820
Reaction score
2,758
Naam ndugu wajumbe wasaalamu,

Leo imekuwa ni siku ya fanaka kwa chama cha CHADEMA Meatu baada ya kuchukua fomu za ubunge na udiwani kwa mafanikio makubwa.

Kuweka kumbukumbu sawa:Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu ina majimbo mawili ya ubunge ambayo ni Meatu na Kisesa.

Jimbo la Meatu kwa sasa lilikuwa chini Salum Mbuzi almaarufu Jambo huku jimbo la Kisesa likiwa chini ya Mhe Waziri Mpina.

Kamanda Mwl Johnstone amechukua fomu kugombea jimbo la Meatu huku Kamanda Francis ambaye pia alikuwa diwani wa kata ya Mwandoya amechukua fomu kugombea jimbo la Kisesa.


IMG_20200813_135604_7.jpg
IMG_20200813_135624_4.jpg
Pia mgombea udiwani kata ya Mwanhuzi ambayi ndipo yalipo makao makuu ya wilaya ya Meatu kamanda Magembe naye pia amechukua fomu leo.
Mshindi halalii ashinde.
 
Back
Top Bottom