Meatu: Komred Mpogolo awaongoza waombolezaji mazishi ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu, Ndg. Enock Ng'wigulu Yakobo

Meatu: Komred Mpogolo awaongoza waombolezaji mazishi ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu, Ndg. Enock Ng'wigulu Yakobo

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
Meatu-Simiyu

KOMRED MPOGOLO AWAONGOZA WAOMBOLEZAJI MAZISHI YA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA SIMIYU.

Naibu Katibu Katibu mkuu wa CCM Bara, Komred Rodrick Mpogolo amewaongoza maelfu ya Wananchi na na Wanachama wa CCM katika mazishi ya aliekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu na Mjumbe wa Halimashauri kuu ya Taifa Ndg.Enock Yakobo Mwigulu yaliofanyika hii leo ktk eneo la Mwanu'hzi wilayani Meatu, mkoani Simiyu.

Katika salamu zake za pole kwa wafiwa na familia, Komred Mpogolo amemuelezea Marehemu Mzee Enock kuwa alikuwa ni mtu mwenye busara,mchapa kazi na askari wa mstari wa mbele wa CCM ktk nyakati zote.Hivyo amewaomba viongozi na wanachama kumuenzi kwa vitendo.

Mazishi hayo pia yamehudhuriwa na Mlezi wa mkoa wa Simiyu,Mwenyekiti wa UVCCM Taifa na mjumbe wa Kamati kuu Komred Kheri James,Wenyeviti wa mikoa,WaNEC,Wakuu wa mikoa na wilaya,Viongozi wachama na jumuiya,viongozi wa dini,watumishi wa umma na wananchi kutoka Maeneo mbali mbali ya Nchi.

"Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe"

IMG-20210226-WA0013.jpg
IMG-20210226-WA0014.jpg
IMG-20210226-WA0012.jpg
 
Huyu mzee 2015(kampeni) nikiwa UVCCM nilifanya naye sana kampeni na alikuwa mtu wa watu sana
 
Back
Top Bottom