Mechanical engineers wa Tanzania wana msaada gani kwa nchi?

Acheni kusingizia serikali, mbona wanasiasa wanatoboa huku mazingira ya kisiasa sio sawa! Mfano Msigwa kachukua Jimbo la iringa mjini bila kuwepo siasa Safi!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
maengineer wa kwetu hawawezi kutengeneza mitambo,ila wamefundishwa ku operate mitambo tu
 
 
maengineer wa kwetu hawawezi kutengeneza mitambo,ila wamefundishwa ku operate mitambo tu
Hicho ndicho ninachojaribu kuwaeleza kuwa waache ukitonga but waende mbali zaidi ili wawe watengenezaji. Kwanini wazungu waweze sisi tusiweze?

Wanasema umasikini wakati uwezo wa kufikiri mdogo. Geuza huo uwezo na ujuzi wako kuwa mtaji wako na si vinginevyo. Ukionesha uwezo wako hakika utasaidiwa.
 

Sasa utukejeli mara ngapi,threads nzima unawakejeli engineers.

Ila wewe si umesema Lawyer ni noble proffession,sasa Wanasheria na wahasibu ktk thread wamefuata nini? Au umesahau kama wewe ndio umewaingiza.

Nani kakwambia wanasayansi US wameanza kuonesha uwezo wao,alafu serikali ikawasupport hebu nipe mfano mmoja tu?
Wenzenu ulaya serikali yao imewawekea Lab kuanzia elimu ya awali mpaka chuo na bado final year project wanafunzi wanapewa hela ya kutosha na kama serikali wakiiona nzuri wanaisupport.Wana center kibao ya kitafiti za maswala ya kisayansi leo TBS kuna bidhaa nyingine wanazipima kwa macho sababu hawan maabara inayojitosheleza.Sasa ikiwa TBS yenyewe hali mbaya vipi huyo Engineers atakuwa na hali gani.Mack Zuckerburg,Bill gates,Steve Jobs tokea wadogo wanazijua Computer,huku TZ mtu Computer anaijulia chuo .

Najua unapayuka payuka siku tembelea kwenye final year presentation pale CoET au CoICT
wakiwa wanafanya projects zao zile za final years tena kwa gharama za mifuko yao ,lkn serikali yako haioni.Hizi mashine ndogo ndogo za kusaga nafaka na kukoboa Watoto wa Mechanical Engineer wamezitengeneza kibao,hizi mashine za kupukuchua mahindi zipo kubao pale CoET,serikali yako inashindwa hata kuzipromoti wahisani wazione.CoICT kuna systems kibao pale ambazo zinaweza kuwa solution kwa taasisi za kiserikali,tena zimefanyiwa tafiti ktk taasisi hizi za kiserikali lkn taasisi na serikali hawazioni,washazoea system ya kawaida wanainunua kwa bilion 1 huku nyingine washapiga,wakati wanafunzi ukiwapa milion 100 wanakutengenezea system uitakayo ww na wataisupport kwa gharama nafuu kuliko hiyo uliyoinunua toka nje.

Kuna madogo wa Computer science UDOM 2014 wamebuni system ya kusimamia kesi mahakamani,ili kupunguza msongamano wa kesi mahakamani na kuondoa mfumo wa kuhifadhi taarifa kwenye mafile mahakamani,wameenda mpaka mahakamani kufanya research lkn mwisho wa siku si mahakama wala serikali yako haijathubutu kuwatafuta wale vijana kuboresha uendeshaji wa mahakama.

Sasa jiulize ikiwa watu historia wanashindwa kufanya research hizi kwenye makabila yetu 126 mila na tamaduni zao,machifu wao na zana walizokuwa wakitumia, je huyu mtu wa Science ndio ataweza.Watu wana idea kibao kuna dogo Mzanzibar kasoma UDOM anaitwa Salim kamaliza 2014 katengeneza Compiler kwa designed zake,lkn serikali yako imeshindwa kumwona.

Wewe siku ukipata muda zamia kwenye hizi fainal year presentation za Engineers CoET,CoICT,DIT,UDOM (Informatics and Virtual Educations) alafu angalia idea za wanafunzi wanavyo ziwasilisha practically,utakuja kugundua idea zipo ila tatizo serikali yako haioni wameng'ang'ania siasa..

Eti Lawyer noble professional,wanashindwa kufanya mambo yao msingi kwa ajili ya taifahili,wamejificha kwenye siasa,kutwa kudai katiba mpya na kulamba miguu ya wanasiasa.Mwisho wa siku wakapigwa Mlimani City kuanzia wanafunzi mpaka maprofesa wao hawajui walicho kisaini.

Hao wahasibu wako wenyewe mda si mrefu watu wa Computer Science,Software Engineering,Computer Engineering,Business Information system watazichukua kazi zao.
 
Tunavyolaumu CCM kama dude hivi wakati ni ndugu zetu kabisa.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huko serikalini si wapo maengineer?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndo umeishia hapo ?

Huyo unayemuona hana msaada, amekuwa na msaada mkubwa sana na kusukuma maisha yako, kitu pekee ambacho haujui ni mazingira yao ya kazi. Engineers wanafanya kazi zao nyuma ya mapazia ndio maana unapata uthubutu wa kuandika unachoandika. Engineers work on things ndio maana hutowaona, political scientists and sociologists wao wanadeal na watu na ndio maana unamuona ana thamani sababu wanapofanya kazi mnawaona na camera zinakuwa pembeni yao kuwamulika.
Kisa hujawahi ingia huko ICU au Theatre ndio maana unaona Daktari Hana maana sio ?

Umewaza juu ya uwekezaji, materials availability, potential buyers wa hizo vitu, market sustainability baada ya Corona kupotea na affordability ?
 
 

Hongereni mkuu.

Vipi umahiri (competence) wenu wako ukoje?

Mkuu naongea hivyo kwa sababu kuna kesi nyingi unakuatana nazo mpaka unashangaa why watu wa kadaa hii wanakuwa hivi? unaweza kwenda hospital ukaambiwa unaumwa hiki kumbe huumwi huo ugonjwa mfano mzuri ni msanii fulani alienda hospital moja hapa TZ akaambwa anaumwa cancer wakati siyo kweli ila alipoenda Kenya, SA aliambiwa tatizo na natumai amepona.
 
Kwa hiyo kesi ya msanii mmoja ambaye hatujui alienda hospitali gani na alikutana na nani ndio anakufanya udharau madkatari tulionao ? Siku nenda kakae pale Moi japo kwa saa moja tu nadhani utaanza waheshimu na iheshimu kazi yao. Siku ukipelekwa Theatre wanapofanyia mtu surgery nadhani utakuja upya na thread hapa ya kuwapongeza Madktari kwa kazi yao iliyotukuka wanayofanya.
 
Halafu Mzungu wa watu akisema tunakuja kufanyia utafiti wa chanjo kwenu, duu!!! Si kelele hizo, ooh mmetuona sisi manyani sio!! Hatutaki. Acheni dharau zenu eboo!! Fanyieni kwenu. Kaaaazi kwelikweli!!!
 
Ukijibu ndio huko nakuprove wrong 👇

1. Naomba uweke hapa ratio ya wageni vs wazawa viwanda vifutavyo

A) Tanga cement

B) mbeya cement

C) Atlascopco

D) Geita gold mine

2. IP reference yako kusema hayo unayoyasema by company names
To be obvious, wengi huko wanafanya kazi katika level ya technicians!!
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Unawafahamu vizuri hao mechanical engineers unotuhumu kuwa hakuna wanachofanya? Unawafahamu vizuri madaktari uliowajumuisha na wahandisi kuwa wanafanya nini? Ni vema walau umetambua umuhimu wa taaluma hizi baada ya kuzuka Corona. Lakini huwatendei haki kuwanyoshea kidole na kuwaacha watunga sera wasio thamini taaluma hizi na nyinginezo kwa maslahi mapana ya wanasiasa. Unakumbuka mhandisi wakati wa Corona. Si wewe tu, hata mechanical engineers walio viwandani hutambuliwa wakati machine breakdown na kuna msururu wa malori nje yakisubiri bidhaa. Wanajeshi tunaona wazururaji tu mpaka siku nchi unaingia vitani ndio utajua umuhimu wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
To be obvious, wengi huko wanafanya kazi katika level ya technicians!!

Sheria ya nchi expatriate wanatakiwa Kuwa GM's, CEO's nk where applicable

Yet bado makampuni machache hawajatekeleza mengi teyari yametekeleza.

Nowadays
Plant managers, managers either electrical, mechanical or preventive or quarry or quality assurance to the bottom need be indigenous..... by country law.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…