Mechi ipi bora ya Simba kimataifa

Dabil

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2021
Posts
6,823
Reaction score
15,293
Kwa mechi tulizoshinda kimataifa ni mechi gani bora wewe ulienjoy? Binafsi kwangu vs Platnums biriani ilipigwa.

Simba vs Nkana 2-1
Simba vs As Vita 3-1
Simba vs Fc Platinum 4-0
Simba vs Red arrows 3-0
Simba vs Orland 3-1
Simba vs berkane 1-0
Simba vs Mimosas 3-1
Simba vs Al Ahly 1-0
Simba vs US Gendamarine 4-0
 
Mimi naona ni ile na kaizer chifs kwa mkapa
 
Hata kwenye zile mechi alizopigwa Khamsa na Al Ahly na As Vita, hakika aliupiga mwingi! Maana kipa Aishi Manula aliokota mpira golini mpaka alichoka.
 
Vs kaizer chief mpaka utopolo walitoka wakisema hiiiii! Bhagosha!
Ila kuna ile ya marudio pia kule Bondeni! Kwa mara ya kwanza tulishuhudia Chris Mushimba Mugalu akicheza kama kiungo mkabaji!

Hakika waliupiga mwingi mpaka basi. Ingawa mwisho matokeo yalikuwa ni ya kukatisha tamaa pamoja na yale matumizi ya ile kitu ya moto.
 
Acheni mambo ya kitoto bhana. Utani unafanyika humu jukwaani! Inakuwaje muwahusishe na wazazi?
Kuna katabia huwa nakaona kwako mkuu na huwa kananifanya nikuone ni mnafiki tu, pale ambapo shabiki wa Yanga Sc anapoanzisha matusi humu kwenye jukwaa huwa unajifanya huoni ila pale ambapo shabiki wa Simba Sc ataamua kuyajibu hayo mashambulizi kwa matusi, ndipo huwa unajitokeza kuonyesha hizi busara zako za kijinga.

Aliyeanzisha kimtusi mwenzake ni shabiki wa Yanga na haukumpa huu wasaa wako, ila baada ya jamaa kujibu ndio imekuuma sana? BINAFSI naungana na huyo aliyemtukana mama wa huyo jamaa aliyeanzisha matusi humu.


JIFUNZE KUWA FAIR.
 
Uko sahihi kabisa. Kuna kale katabia ka kuoneana aibu kwa sababu tu ya kufanana mlengo. Na kama ndiyo unafiki wenyewe, basi nakiri na mimi kumbe ni mnafiki kwa kiasi chake.

Lakini kiukweli tujitahidi tu kutaniana kwa kipimo. Hata wale mashabiki wenzangu wa Yanga pia wabadilike. Hii mambo ya kutukanana matusi ya nguoni, kuwatukana wazazi wetu! Nadhani siyo poa hata kidogo.

Huwa napenda tuishie tu kwenye utopolo, umbumbumbu, umakolo, nk.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…