Mechi ya Azam FC Vs Kitayosce imemalizwa kabla ya muda baada ya Kitayosce kubakiza wachezaji pungufu uwanjani

Mkuu hakuna cha ratiba kuvurugika, kwani ushajua team zetu mfano zikavuka hatua za awali za mashindano ya kimataifa unadhani ratiba haziharibiki / kuvurugika? Uliona wapi match official ya ligi ikachezwa wachezaji hawajatimia? Au unadhani ndondo hiyo kaka?
 
Hapo ni sheria za FIFA zimefuatwa ndo maana wakaingia hao hao 8,wangekuwa pungufu Zaidi mechi isingechezwa ndo maana walijifanya kupata injury makusudi ili mechi isiendelee.

Kuhusu viporo vya kimataifa inajulikana, sidhani kama kulishatokea viporo Zaidi ya 3 na zinaisha vizuri,sasa umwekee viporo mtu kwa uzembe wake na siyo mechi ya kimataifa?na wamekumbushwa .
 
Mkuu unaweza nisaidia hiyo sheria ya FIFA inayoruhusu match official kuchezwa / kuanza ikiwa team pinzani haijakamilika wachezaji ili nami nijifunze?

Kama sikosei au nitakuwa sahihi kuna ule msimu simba ana viporo 8+ unaposema hudhani kulishatokea una uhakika na hilo mkuu?

Kimataifa inajulikana ndio match zipo na zitachezwa, nilisema hiyo point baada ya wewe kusema kuwa kuhairisha match au kusogeza match mbele itavuruga ratiba, ndio swali langu likaja kuwa kuna match za international itakapotokea team zetu zitaendelea na hatua za mbele zaidi, je zenyewe hazivurugi ratiba?
 
Mkuu nimekuelewa,lakini kama hivo inawezekana kwanini waliingia uwanjani na kucheza mechi?
 
Sasa kama magoli yanahesabika ni mawili tu kwanini Feisal kapewa mpira?
 
Hivi Kigwangala yuko wapi? Kelele zote zile za kumsakama Mo Dewji, leo anashindwa kuiokoa timu iliyo kwenye mkoa wake?
 
Japo sheria inataka hivyo ila ili kulinda heshima ya ligi yetu TFF ilitakiwa iahirishe hii mechi. Tumejivua nguo, hadi media za nje zinatangaza hii kitu.
Yan uhailishe mechi kisa timu moja imeshindwa kukamilisha usajili nawashakumbushwa sana tu... Unakumbuka mwaka juzi yanga ilivyopigwa nje ndani na rivers united ya Nigeria wachezaji wakigeni akina mayele hawakusafili natimu kisa hawakukamilisha vibali vyao sasa ulitaka mechi ihailishwe kisa yanga
 
Tukisema pale TFF hakuna watu wa mpira kuna kikundi tu cha wahuni mnatuona hatuna akili / tunahate sana

Bongo wale jamaa wa Guiness world record hawajapashtukia tu, kuna recoed za kutosha na balaa sana ambazo huwezi pata mahala pengine
Mpira siku hizi umevamiwa ma wanawake basi shida tupu yani ujinga ufanywe na timu ila lawama wanapewa TFF.
 
CAF, TFF..
 
Sasa kama magoli yanahesabika ni mawili tu kwanini Feisal kapewa mpira?
Yule kiongozi wa Bodi ya ligi kueleza vizuri sheria yao imekaaje. Kulingana na sheria ya TFF kama timu itacheza pungufu ya wachezaji 7, mchezo utafanyika na timu yenye wachezaji 11 itapewa ushindi wa point 3 na magoli 3 ikiwa tu mchezo umevunja wakati timu hazijafungana au zikiwa zimefungwa chini ya magoli 2 na kama zimefungana magoli 3 na kuendelea itapewa magoli hayo na magoli yatahesabika Halali.

So mpaka game ya jana imefungwa, AZAM alikuwa ana magoli 4 ndio yakahesabiwa mkuu. Hayo ya magoli 2 na points 3 ilikuwa zamani sana wakati nacheza ndondo.
 

Kuna kitu kinaitwa BUSARA mkuu
Akina Mayele walikua wangapi vibali vilichelewa? zingatia huko ni CAF na Yanga ilikua ina majina zaidi ya 30 so why CAF iahirishe?

Hapa tunazungumzia wachezaji 8 tu mkuu na TFF wanalijua hilo
Hawa kwa ujinga wao na ugeni wao una ahirisha game kisha unawatwanga faini wakae sawa na maisha yanakwenda

Yaani kweli TFF unapeleka mafisa wako kusimamia mechi huku unajua kabisa timu yako moja ina wachezaji nane tu?
(Kwanza kanuni inaruhusu kweli timu kuanza ligi ikiwa na wachezaji 8 tu)

Busara ya kijinga tu ili hairisha mechi ya Simba na Yanga kupisha uzinduzi wa kitabu cha mwinyi wakati watu wamejaa uwanjani wanasubiri timu ziingie
 
-Timu imesajili wachezaji 30 wageni ni 12 wazawa 18 sasa hao wazawa 18 walikwenda wapi.
-Timuzote za ligikuu zinatakiwa kuwa na timu za vijana za U-17 na U-20 na wachezaji wa timu za vijana wanaruhusiwa kucheza mudawowote wakipangwa na kocha .Je walikua wapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…