Nilifuatilia mechi ya jana Simba dhidi ya Mtibwa na ninawashauri Klabu ya Simba kama ifuatavyo:- Licha ya kucheza vizuri lakini bado kuna tatizo na mlinda mlango. Manula siyo maakini hata kidogo na lile goli la jana kama kipa angekuwa maakini lile goli lisingetingisha nyavu. Changamoto lingine la Manula ni kimo chake. Kwa kimo ni mfupi na kwa kawaida mlinda mlango anatakiwa mtu mrefu na machachari. Nawashauri mfanyie kazi hizo changgamoto. Timu ni nzuri sana na hata kocha asilaumiwe ni kocha mzuri sana.