Mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya JKT Tanzania ambao awali ulihairishwa baada ya mpinzani wetu kupata ajali sasa umepangwa kuchezwa Disemba 24, 2024 saa 10:00 jioni katika Uwanja wa KMC Complex. Mchezo huu awali haukuchezwa kutokana na JKT Tanzania kupata ajali ya gari na baadhi ya wachezaji wao kuumia.