Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Bodi ya Ligi imeahirisha mechi kati ya Simba SC na JKT Tanzania kufuatia ajali iliyolikumba kikosi cha JKT Tanzania. Ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 1:00 asubuhi baada ya basi lililowabeba wachezaji na wafanyakazi wa JKT Tanzania kuacha njia na kuanguka mtaroni, na kusababisha majeraha kwa baadhi ya wachezaji na wafanyakazi.
Soma, Pia: Basi la Klabu ya JKT Tanzania lapata ajali, Wachezaji 12 wapo chini ya Uangalizi
Kufuatia kuahirishwa kwa mechi hiyo, Klabu ya Simba sasa inajiandaa kwa nguvu zote kuelekea Kigoma kwa ajili ya mchezo dhidi ya Mashujaa FC utakaochezwa Novemba 01.
"Baada ya kuaghirishwa mchezo wetu dhidi ya JKT Tanzania, nguvu yote sasa tunaielekeza Kigoma kwenye mchezo dhidi ya Mashujaa Novemba 01" - Ahmed Ally, Meneja wa Habari na Mawasiliano.