Mechi ya taifa stars

jangala22

Senior Member
Joined
May 20, 2021
Posts
165
Reaction score
141
Habar wanajamvi nauliza mechi ya leo ya taifa stars vs Uganda inarushwa channel ipi
 
Huwa sina mzuka wa kuangalia taifa staa .maana najua hatutafika popote.Bora nikomae kwenye vilabu kama simba,yanga nk
Hii timu ina haribiwa na siasa za kijinga za ccm,juzi kama umesikia naibu waziri wa Sanaa,utamaduni na michezo anakwambia kwenye michezo wametenga Tsh 183 milioni,hebu fikiria na hapo hiyo hela inahusu timu zote yaani ya wakubwa,under 20,under 21 na timu ya wanawake!.
Hii nchi ina vituko mnooooooo!
 
Habar wanajamvi nauliza mechi ya leo ya taifa stars vs Uganda inarushwa channel ipi
Taifa Stars inaongoza goli moja bila.

Goli la Saimon Happygod Msuva, dk 29.

Mpira utaisha muda siyo mrefu.
 
mechi imeoneshwa na TV ya Sports ya Libya, nimeangalia tumecheza kwa akili sana wachezaji wa Simba wanaotuchomeshaga wote hawamo ni Mzamiru na Kakolanya tu ndo wamepenya kwa kutumia kamati za ufundi za bibi zao na timu imeshinda Tanzania 1 Uganda 0

 
Tumeshinda?? Si nimesikia wachambuzi wetu wa soka wakisema hatuwawezi Uganda hata kwa dawa!
 
mechi imeoneshwa na TV ya Sports ya Libya, nimeangalia tumecheza kwa akili sana wachezaji wa Simba hawamo ni Mzamiru na Kakolanya tu timu imeshinda Tanzania 1 Uganda 0
Hebu tupe uchambuzi? Maamuzi ya kocha yalikuwa sahihi? Kwa mtazamo wako?....Na je kiwango umekionaje kimeridhisha?
 
Hebu tupe uchambuzi? Maamuzi ya kocha yalikuwa sahihi? Kwa mtazamo wako?....Na je kiwango umekionaje kimeridhisha?
timu bado ila mwelekeo umeonekana. tumejilinda zaidi badala ya kushambulia. wachezaji wamejituma sana maana hawana majina makubwa
 
Hiyo hela inapwaswa kuwa match winning bonus ya mechi mbili tuu za timu kubwa.
Tuna utani mwingi sana sie
 
Habari Mleta Thread,Mechi ya Leo itakuwa live?
Na je hiyo channel uliyoangalia inapatikana kwenye Kisimbuzi kipi??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…