Mechi ya Watani wa Jadi....

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,258
Nimeangalia timu zote mbili yaani Yanga na Simba



  1. Timu zote zinacheza mchezo wa pasi ndefu yaani high balls ingawa Yanga wanaonekana kuwa na advantage ya mchezo huu kwa sababu wana washambulizi karibu wote wenye kasi hasa Ngoma. Msuva na Tambwe ilihali simba anayeonekana kuwa mwiba kwa staili hii ni Hamis Kiiza tu kwani Ajib na Mwalyanzi wanapoozesha
  2. Timun zote zinakaba njia ingwa simba wanaonekana kuwa na advantage kwani wana viungo wajanja na wepesi kidogo pale kati ilihali Yanga wanapoozesha kidogo na wana watu ambao hawana concentration ya muda mrefu kwani hii ni aina ya mchezo unaohitaji mental than physical presence on the field (zonal marking)
  3. Defence ni nzuri kwa timu zote ila Yanga wana advantage ya experienced defenders and goal keeping kitu ambacho simba wana lack hasa Manyika, kwa goli walilofungwa simba jana uzeofu wa kipa ulichangia kwani hakusema na walinzi wake na aliwahi kutoka walinzi wakajenga imani kumbe hakuwahi tukio na akapigwa tobo
  4. super sup za timu zote ni nzuri sana ingawa sijaipenda sub ya Ndaw huenda Lyanga angeongeza nguvu kuliko Ndaw mfano utaona kabisa anapoingia Malimi kuna pressure flani inaongezeka na hata Msuva akianzia benchi lango la adui linakua hatarini muda mwingi
  5. ........................................
  6. matokeo?
 
Tatizo la Yanga ni moja... Timu hata ikwa nzuri kuliko Simba, ikikaribia mechi tu, wachezaji wa Yanga wanaingia hofu na siku ya mechi wanakuwa wepesi kutoka mchezoni. Mfano hadi sasa Yanga itabidi wamtegemee Barthez tu golini kwani Dida alishakataa kupangwa mechi dhidi ya Simba. Jambo hili la hofu limeenea kwa wachezaji karibu wote ukiondoa wazimbabwe ambao hawaijua bado pressure ya Dar Derby, ila wakishajua reaction ya washabiki baada ya mechi, hata nao wataanza kuingiwa na hofu mechi zijazo
 
Asante kwa uchambuzi mzuri.

Ktk mchezo ujao, Yanga inatarajiwa kubebwa na uzoefu hasa ktk defence, ukubwa wa kikosi (squad depth) hasa kwenye eneo la ushambuliaji, lkn pia Ngoma mwenyewe ni factor inayojitosheleza kutokana na upambanaji, kasi na uchezaji wake usiokuwa na uchoyo kwa wenzake. Eneo la ushambuliaji la Yanga ni tishio sana na kwa kweli laweza kuwa eneo bora zaidi ktk ligi hadi sasa. Walioko uwanjani na walioko benchi wote ni moto bati. Kasi ya viungo wa pembeni nayo pia ni silaha tosha dhidi ya Simba. Yanga pia inaonekana kuwa na kikosi kilichokaa muda mrefu na kocha anayeifahamu timu kwa kiwango kizuri. Hizi ndizo silaha za Yanga kuelekea 26/9/2015

Kwa upande wa Simba, eneo ambalo ni hatari zaidi ni kiungo na stamina ya kutosha. Simba wana kiungo bora sana chenye mchanganyiko mtamu. Mchezaji Said Ndemla anajitokeza kama turufu ya Simba dhidi ya Yanga kwa uwezo wake wa kukaba, pasi ndefu na fupi, work rate ya kurishisha na unyumbulifu. Aidha, ana ujasiri wa kupambana na yeyote kwa hiyo anasaidia sana wakati wa ukabaji na uchezeshaji. Hupati wachezaji wengi wanaoweza kukupa vitu hivi kwa pamoja. Uwepo wa Mwinyi Kazimoto kwenye kiungo cha juu na Justice Mzabvi kwenye kiungo cha chini na 'uchawi' wa Ndemla ni silaha hatari sana kwa Yanga hasa unapokuwa na washambuliaji wa aina ya Mgosi, Kiiza na Mwalyanzi kwa kasi, unyumbulifu na uwezo wa kufanya lolote wakati wowote
 
nimekukubali pia

kuna mtu jana alikua anajaribu kumfananisha Ngoma na Yule Mliberia lakiji ukweli ni kwamba Ngoma ana vitu vya ziada ambavyo ni speed na stamina yule Mliberia ana skills zaidi za mpira lakini alikua na vitu vini sana ilihali Ngom yeye analijua lango tu

huyu mido mzzim wa YANGA anajua sana high balls na ananikumbusha Chuji

mzimbabwe wa simba wamelamba dume; nimemuangalia mechi nyingi kiukweli yupo kazini tofauti na watu kama simon na ajibu ambao wanacheza kama wapo mazoezini, iwapo kama ni kweli Mkude atarudi dimba la chini la Majabvi akasogea kulia kwa kukabia ndani basi Yanga watautafuta sana mpira

kessy wa jana hakua kwenye ubora wake ila staili ya yanga ya kutokea pembeni inahitaji mabeki wenye kasi pia na akili kama shabalala na kessy hata emey ameonesha kuwa na kasi sana tofauti na Twite anayechoka haraka

itakua mechi kali kwa kweli ukweli kwamba zinakutana zikiwa kwenye top positions japo hazijakutana na manguli wengine wa soka


 

asante TWAWEZA kwa tathimini lakini hujatushirikisha kabla hujatoa mada
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…