Hakuna kitu kibaya kama umeenda Taifa asubuhi sana, pengine umekunywa chai na andazi moja. Jua lako Mchana kutwa.
Jioni unashangilia dakika 90 halafu Timu yako inafungwa, mpira ukiisha inabidi upige mguu mpaka Buguruni ili upate usafiri wa kwenda Mbezi mwisho. Hayo ni mateso makubwa, bora Yanga ashinde hii mechi