Grey256
JF-Expert Member
- Sep 1, 2016
- 1,236
- 2,600
Habari wanazengo,
Kuna kitu nimejaribu kukifanyia utafiti kuanzia kwenye level ya mimi binafsi,marafiki na jamii ya wapenda soka inayonizunguka na mwishoe nikapata jibu ambalo nimetamani kushare nanyi pamoja na wadau wa michezo kwa ujumla.
Mimi binafsi ni shabiki mkubwa wa timu moja wapo kati ya hizo na katika miaka kadhaa iliyopita nilikua naweza kuhudhuria karibia mechi zote za timu yangu ndani ya msimu zinazochezwa taifa au hata za wapinzani wetu hilo limekuja kubadilika tangu walipoanza kuzipeleka mechi za timu hizi mbili saa moja usiku kiukweli nilijaribu kwenda msimu uliopita na huu mechi kadhaa ila imefika wakati imebidi nikubali kuwa nimeshindwa.
Hali hii nimeiona pia kwa mashabiki wenzangu wengi wa mpira ambao nilikua nikienda nao au nikikutana nao uwanjani kila ninapoenda. Sababu kuu ambayo nimeiona ni hali ya usafiri,umbali,miundombinu na usalama wa baadhi ya maeneo tunayotoka kuwa ni kikwazo kwa mtu especially sisi wenye vipato vya kati kuhudhuria mechi za usiku mara kwa mara maana unakuta mtu unakaa Boko mpira unaisha saa 3+ hapo ndo uanze kutafuta usafiri wa kurudi kwenu,hekaheka hizo unaweza kuta unafika stand ya Boko saa tano au sita usiku hapo bado hujatafuta boda (gharama ya ziada) au haujatembea kwenda kwenu mida ambayo kiusalama sio sawa.
Nadhani hizi timu au bodi ya ligi zinaweza kupitia tu takwimu zao za mahudhurio wakati ule mechi zinachezwa saa 10 jioni na sasa natumaini wataona tofauti kubwa sana. Kama wameweka ratiba hivi kwa matakwa ya mwekezaji (Azam tv) na analipa vizuri basi sawa ila kama kuna haja ya kuimprove mapato ya mlangoni nadhani wafikirie kuturudishia ratiba yetu ya saa 10-11 jioni mida ambayo wananchi wengi tunaweza kwenda uwanjani na kurejea majumbani kwetu mapema kwa usalama na bila gharama za ziada.
Nawasilisha.