Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, TPLB imewaagiza makamisaa wote wa mechi za mtoano na Ligi Kuu ya Vodacom kuwa na dakika moja ya maombolezo katika kila mechi itakayochezwa kwa kipindi cha maombolezo.
Kabla ya mechi kuanza watu wote watatakiwa kusimama kwa dakika moja kuonyesha heshima kwa na kuombleza kifo cha Rais wa awamu ya tatu wa Tanzania, Benjamin Mkapa.
Utaratibu huu utakuwa katika kipindi cha siku saba kama zilivyotangazwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli.