Medani za Kijeshi

Medani za Kijeshi

King Gaddafi

New Member
Joined
Jan 1, 2024
Posts
2
Reaction score
10
Je, akikutana Afisa wa JWTZ mwenye nyota tatu (3) na Afisa wa polisi mwenye nyota tatu (3), nani atatakiwa kumpigia mwenzake Saluti na kwa vigezo vipi?
 
Wenyewe wanajua kipi wanapaswa kufanya pindi wanapokutana maana kwa majukumu yao hukutana mara kadhaa kwenye shughuli za ujenzi wa Taifa.
Swali, je, wewe unataka kujua ili iweje? Kwanza una uraia wa nchi gani?
Kimsingi wanajeshi wanaweza kutangaza hali ya hatari na pua la yeyote lisitokeze nje uwe na nyota 3 ukionwa during that time unakula kichura

NB: Sijajibu swali lako. Nilikuwa nachombeza tu
 
Je, akikutana Afisa wa JWTZ mwenye nyota tatu (3) na Afisa wa polisi mwenye nyota tatu (3), nani atatakiwa kumpigia mwenzake Saluti na kwa vigezo vipi?
Jiulize wanajeshi wenye vyeo sawa au polisi wenye vyeo sawa ni yupi anakiwa kupiga salute kwa mwenzake?

Jibu utakalopata lina-apply pia kwa polisi na mjeshi wenye nyota tatu (ndivyo ulivyouliza) wakikutana.
 
Kuna yule aliyewahi kuwa mkuu wa jkt halafu akatupwa mkuu wa mkoa Kagera sasa sijajua ni kukomoana ama nini.
 
Kwa kawaida, saluti hupigwa kwa kuzingatia cheo, bila kujali taasisi. Kuna sheria na kanuni za kijeshi Kwa ujumla, katika hali nyingi, Afisa wa Polisi ndiye atakayempigia saluti Afisa wa JWTZ. Hii ni kwa sababu yq kutambua ukubwa wa jeshi la wananchi.

Zile bakabaka zimebeba sare ya majeshi yote mfano; jeshi la polisi, uhamiaji, magereza nk. Kwaiyo kiprotocal huyo jamaa wa polisi inabidi aangushe saluti tu.

Japo mazingirq pia yanaweza kusababisha afisa wa jw kumpigia salute huyo mwenye cheo kama iwapo atamkuta kwenye eneo lake la kazi.
 
Kwa kawaida, saluti hupigwa kwa kuzingatia cheo, bila kujali taasisi. Kuna sheria na kanuni za kijeshi Kwa ujumla, katika hali nyingi, Afisa wa Polisi ndiye atakayempigia saluti Afisa wa JWTZ. Hii ni kwa sababu yq kutambua ukubwa wa jeshi la wananchi.

Zile bakabaka zimebeba sare ya majeshi yote mfano; jeshi la polisi, uhamiaji, magereza nk. Kwaiyo kiprotocal huyo jamaa wa polisi inabidi aangushe saluti tu.

Japo mazingirq pia yanaweza kusababisha afisa wa jw kumpigia salute huyo mwenye cheo kama chake iwapo atamkuta kwenye eneo lake la kazi.
Maua yako 🌹
 
Endapo maofisa wa majeshi tofauti wenye cheo kinachofanana (equivalent) wakakutana, busara hutumika zaidi. Seniority itazingatia jeshi la ofisa husika. Officer anayetoka jeshi junior basi ataanza kumsalute officer anayetoka jeshi senior., kwa mpangilio wa
Jwtz
Police
TISS
Magereza
Fire
Uhamiaji
 
Endapo maofisa wa majeshi tofauti wenye cheo kimoja (equivalent) wakakutana, busara hutumika zaidi. Seniority itazingatia jeshi la ofisa husika. Officer anayetoka jeshi junior basi ataanza kumsalute officer anayetoka jeshi senior., kwa mpangilio wa
Jwtz
Police
TISS
Magereza
Fire
Uhamiaji
TISS ni jeshi?
 
Polisi mwenye Cheo Cha Afisa atasalimiwa kwa heshima ya salute pale Askari jeshi au Afisa aliye chini yake akiwa na shida ya msaada wa kipolisi tu 😂 Nevertheless Senior ni senior tu kumjua sasa ndio haipotezwi muda.
Jibu limekaa vizuri hope wameelewa

Many thanks Lt.Col
 
Je, akikutana Afisa wa JWTZ mwenye nyota tatu (3) na Afisa wa polisi mwenye nyota tatu (3), nani atatakiwa kumpigia mwenzake Saluti na kwa vigezo vipi?
Form two jamvini wakisubiri matokeo wanasumbua hadi huku.
 
Back
Top Bottom