Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 59,045
- 94,974
Unajua hawa watu wakishakuwa madarakani huwa wanajisahau sana. Lakini wanaweza mfanyia Slaa vituko vya kila aina na siku ya siku wakakuta ndiyo Rais. Sijui Tido ataficha wapi uso wake usio na haya katika kuwalinda mafisadi. Tido anatakiwa awe makini sana na mambo anayoyafanya TBC. Ni vema atambue kwamba TBC ni television ya UMMA na inaendeshwa kwa kodi zetu, siyo television ya CCM ile. Ni vema akaitumia vizuri kwa maslahi ya watanzania wote ambao wavuja jasho ili kumlipa yeye mshahara.Kuhusu TBC mimi sasa wala sina doubt tena kuwa inatumika kwa maslahi ya CCM, nami nilikuwa najiuliza sawli kama hili hivi kwanini TBC wanaonesha tu mchakato wa wagombea ubunge kupitia CCM ina maan vyama vingine havifanyi michakato hii! nilikuwa kidogo nishawishike kuwa vyama vingine havina michakato, ila wazo hili lilifutika baada ya kusikia kule Mbeya Chedema walikuwa nao wanakura za maoni juu ya wagombea wao lakini ajabu TBC wala sio tu kulitangaza hata kugusia tu juu ya mchakato huo! Kiboko ni pale juzi Makamba alivyokuwa akiongea na waandishi wa habari, TBC walionesha kwenye taarifa ya habari, na kama haikutosha wakaona waweke kabisa kipindi maalum,! sasa ukajiuliza hivi huo UMAALUM wa kipindi kile ulikuwa wapi? Tido na TBC yake waelewe tu ipo siku historia itawahukumu na unafiki wao!
Nimefuatilia kwa karibu sanani vyombo vingapi viliandika kuhusu Dr. Slaa kule Arusha na jimboni kwake juzi ilee, lakini ukweli ni kwamba ukiacha kwa upande wa TV stations; Channel Ten na ITV hawa wajumbe wengine kama TBC hawakuonyesha kabsaa, nikasubiria niione siku yake ya pili labda walikuwa wanafanyia editing, wapi!!!
Wadau, hii ni kampeni au ni kwamba TBC na baadhi ya magazeti hawana wawakilishi kule Karatu na Arusha??
Nisaidieani
Lakini Tido mbona alipokuwa BBC alikuwa makini sana na alijizolea sifa kemkem, lakini leo hii anafanya madudu! Imekaaje hii wajameni? Huyu Tido wa sasa siyo yule wa zamani. Hawafanani kabisa. Tido wa enzi za BBC uko wapi? Rudi bana!!