Mwande na Mndewa
JF-Expert Member
- Feb 26, 2021
- 1,117
- 3,153
MEI MOSI NA MFUMUKO WA BEI; NINGEPUNGUZA PAYE KAMA RAIS MAGUFULI.
Leo 21:30pm 02/05/2022
Hayati Rais John Pombe Magufuli,alipunguza kodi katika mishahara kwa Wafanyakazi kutoka asilimia 11 hadi asilimia 9,huku wafanyikazi kote duniani wakiadhimisha sikukuu ya wafanyakazi,nchini Tanzania, wafanyakazi walikuwa na kila sababu ya kutabasamu kwa punguza la kodi katika mishahara yao,hivi ndivyo akili ya "problem solving leader" inavyopaswa kufanya kazi.
Mfumuko wa bei unapotokea,mafuta yamepanda bei,kila mmoja anafahamu mafuta ni nini katika uzalishaji!! sasa kama uzalishaji wetu unategemea mafuta, ina maana automatically gharama za uzalishaji zitapanda na kusababisha kitu kinachoitwa "Cost Push Inflation".
1. Bei ya mafuta soko la dunia imepanda,
2. Tukaongeza tozo kwenye bei ya mafuta ambayo tayari yamepanda!
Matokeo yake: Bei ya Juu ya Mafuta Soko la Dunia + Tozo kwenye Mafuta nchini = Bei ya Juu ya Mafuta Nchini!!
-Mlaji wa mwisho ndio mlipaji wa ongezeko la bei,Je tunamfidia vipi mlaji wa mwisho ambae ni mwananchi!?
Katika hotuba ya kuadhimisha siku ya wafanyikazi,Hayati Rais Magufuli alitangaza kupunguzwa kwa kodi ya mapato PAYE kutoka asilimia 11% hadi asilimia 9%.Hii iliamaanisha kuwa kila mfanyakazi atapata ongezeko la mapato yake kwa asilimia 2%.na kwa hakika kila mfanyakazi akapata ongezeko la 2% kutokana na punguzo la kodi katika mshahara wa kila mfanyakazi,hii ndio njia sahihi ya kuongeza mshahara wa mfanyakazi bila bidhaa kupanda bei,hautumii neno "naongeza mshahara" bali unatumia neno "napunguza kodi katika mishahara ya Wafanyakazi" Hayati Rais Magufuli alikuwa "genius" na mshindi kwa hili.
Nimpongeze Mama kwa neno lake "jambo letu lipo,mahesabu yanaendelea" lakini angeweza kupunguza kodi katika mishahara ya Wafanyakazi bila kuwashtua wafanyabiashara kuongeza bei katika bidhaa zao,nikimnukuu Rais Magufuli alisema "ziko namna nyingi za kupandisha mishahara ikiwemo kupandisha madaraja watumishi na kupunguza kodi ya wafanyakazi PAYE,hivyo serikali imeamua kutumia njia hii na watumishi wote wananeemeka".“Mtu anakuja anasema mbona hamjapandisha mishahara?, ukishampandisha Mtu daraja mshahara wake haubadiliki?, tumerekebisha PAE kutoka 11% hadi 9%, tumelipa malimbikizo ya Wafanyakazi zaidi ya Bil 500 hiyo sio fedha!?”- JPM akiwa Mara
Nimalizie kwa kusema vitu Nionavyo shillingi yetu ipo vile vile kama kushake ni kidogo sana,Kilichopo ni Cost-Push Inflation inayosababishwa na kupanda kwa gharama za uzalishaji,napinga wanaosema Demand-Pull Inflation inayosababishwa na kuongezeka kwa demand ya bidhaa.Sasa tujiulize swali, Je njia zinazotumika kuzuia mfumuko wa bei hapa nchini ni salama kwa uchumi wa mtanzania mmoja mmoja?
-Lipo tatizo kwenye kununua bidhaa toka nje ya nchi "Much Imports" kuliko kuuza bidhaa nje ya nchi "Exports".
Ni muda mrefu umepita hatujawa tegemeo kuu la bidhaa fulani Specific Duniani (Parachichi,Zabibu,Mchele,Soya,Arizeti,Viazi) jambo ambalo lingefanya currency yetu kuwa na thamani na kwa kuwa tunategemea dola tukipandisha thamani shilingi kwa ku-Export basi dola ingeweza kubadilishwa kwa kiwango cha kawaida kwa kuwa Demand ya Shillingi yetu kama foreign Currency kwenye Trade ingekuwa kubwa kwa uhitaji wa vitu tunavyolima mfano Parachichi.
Niwaambie ukweli Watanganyika, Wazanzibari kwa neno moja Watanzania wenzangu! Taifa linalozalisha vyema halina Inflation kubwa ya kustusha mpaka katika very special circumstances mfano uwepo wa vita vya sisi wenyewe kwa wenyewe,tuchukulie mfano Urusi inazalisha gesi na mafuta dunia inawategemea,inaendesha vita kuipiga Ukraine na maisha yao yanakwenda kama kawaida.
Nifunge mjadala kwa kusema nimefurahishwa kwa kutoongezewa mshahara wafanyakazi nikirejea ushauri nilioutoa hapo juu,nawaomba wasiwaongeze watu mshahara,ila tujiulize swali lifuatalo;- Je, ni kweli uzalishaji wa bidhaa unakwenda sawa na uhitaji wa bidhaa uliopo? Maana mshahara ukiongezeka mahitaji ya mtu nayo yanaongezeka,asiyekunywa bia nae atataka anywe bia na asiye na gari na atanunua gari, Tukumbuke ya kwamba increase in income lead to increase in demand and it may lead to increase in price if suppy remain constant,kama tutaongeza mshahara basi bei itaoongezeka na tutaukaribisha mfumuko wa bei zaidi na zaidi,ninachoshauri marupurupu yaongezeke kwa Wafanyakazi ila sisemi kwamba watu wajilipe safari za kwenda Semina Uingereza,kabla ya kwenda Uingereza wanaenda kufanya shoping Ufaransa (outfit) baada ya shopping wanaenda kucheki afya Ujerumani wakitoka Ujerumani wanaenda Ontario Canada kufanya small gathering "assembly" kisha wote wanapanda ndege moja kuelekea Uingereza,tusifanye hivyo,tutakuwa tumerudi enzi zile za kupishana angani kama kumbikumbi.
Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854
-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master of Leadership and Management.
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.