Mei Mosi: Ni nini unafurahia kama mfanyakazi

maramojatu

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2012
Posts
2,372
Reaction score
3,108
Wana JF,

Wengi sisi ni wafanyakazi sehemu na idara mbalimbali. Kesho ni siku yetu ya kufurahia na kukumbushia haki zetu.

Kama mfanyakazi ni kitu gani kinakufurahisha kwenye kazi yako.

Kwa mimi ni ile recognition ya msimamizi wangu eneo la kazi.
Je wewe?
 
Wanataka kuongezewa mishahara ila ufanisi upo pale pale
 
Week ends and public holodays.kwangu hiyo ndiyo starehe kubwa
 
Kuwa na usimamizi mdogo kazini baada yakuwa nishaelekezwa kazi na kupewa muda wa feedback kwa kile nilichoelekezwa. Hii namuhakikishia mwajiri naweza kuaminika kutekeleza majukumu yangu kwa ufanisi.
 
Wanataka kuongezewa mishahara ila ufanisi upo pale pale
Ufanisi ni sifa moja Kati ya zilizopo ambazo hufanya mfanyakazi akaongezwa mshahara.
Ikiwa ufanisi ndio kigezo pekee....
Bunge lina ufanisi wa viwango vipya vya juu ukilinganisha na mabunge yaliyopita? Mbona wao wanajiongezea hata kabla ya mei Mosi au wao hawaingii kwenye hii category.
 
Productivity vipi kama unafikiria weekends tu
Hayo ya productivity ni ya upande wa mwajiri zaidi kuyafurahia. mimi kwangu nafurahia zaidi mwisho wa mwezi.mwajiri haijawahi kuwa rafiki wa kweli na mfanyakazi. mwajiri ni kama mchepuko.Anakupenda tu pale unapoweza kumfanyia kazi.ila siku ukiwa na dharura labda ngonjwa anaishiwaga uvumilivu haraka zaidi.ukifa next day nafasi yako iko kwenye gazeti inatangazwa.Si ushauri mzuri sana kuipenda kazi yako.kama unaweza tega kidogo ili upate muda wa kufanya mambo yako binafsi.hayo ya binafsi yana uvumilivu kidogo
 
Hao tayar wana access ya kujiongezea, mm nasemea Hao wngn ambao hawapo kwenye access hy, hata hvy ukishaajiriwa serikalin Hakuna haja ya kuongeza ufanisi.
 
Wanataka kuongezewa mishahara ila ufanisi upo pale pale
ufanisi utatoka wapi.wakati stress za madeni na vikoba vinawachanganya na mshahara mdogo.wamwage hela waone watu watakavyojituma
 
ufanisi utatoka wapi.wakati stress za madeni na vikoba vinawachanganya na mshahara mdogo.wamwage hela waone watu watakavyojituma
Kwamba kipaumbele kiwe kuwamwagia pesa watumishi tuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…