Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametangaza kwa masikitiko kifo cha Meja Jenerali Martin Shiminzi Busungu (Mstaafu), kilichotokea tarehe 24 Disemba, 2024 majira ya saa 10:15 jioni wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Enzi za utumishi wake Jeshini Jenerali Busungu aliwahi kushika madaraka mbalimbali yakiwemo Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa mwaka 2018 hadi 2019.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, Kanali Gaudentius Gervas Ilonda, taarifa za utoaji wa heshima za mwisho kwa marehemu na shughuli za mazishi zitatolewa baadaye.
Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali Pema Peponi, Amina.