Melchizedek na utata unaomzunguka

Yesu alipokuja duniani alikuja katika 4m ya mwili
Na utukufu na baadhi ya mamlaka yake aliyaacha Mbinguni...

Na hapo tunapata sababu ya yeye kujibu vile

Una uthibitisho wa kimaaandiko kuwa Yesu aliacha "baadhi" ya mamlaka yake mbinguni?

Lete andiko la kuthibitisha hivyo, siyo unaleta "dhana", "fikra zako", "falsafa" au "connecting dots"

Huko mbinguni hayo mamlaka alimwachia nani?, na huyo aliyemwachia unauthibitisho gani kama kakubali kumrudishia au kamkatalia?. Maana kwa mujibu wa bible nyakati nyingine Siyo yote Yesu aliyoomba alipewa kwa mfano aliomba anusuriwe kutoka kwenye kikombe cha kutundikwa msalabani lakini akafungiwa vioo!. Sasa huko mbinguni una uhakika gani kuwa hajafungiwa vioo kurudishiwa mamlaka yake?- Au hayo mamlaka aliyaficha mahali wakazi wa huko wasiyaone ili pindi akirudi tu ajivike fasta?

Wenzako wanakwambia Yesu alipokuwa duniani alikuwa Mungu kamili na Mtu kamili at the same time! wewe unasema la hasha Hapa alikuwa Mungu mwenye mamlaka baadhi tu!.

Sasa basi nikwambie, ukishaexist katika any point ya Universe at any time bila kuwa na mamlaka kamili ya uungu maana yake Hukuwa Mungu wa milele, maana mamlaka ya Mungu ni ya Milele popote pale alipo!.
Hilo peke yake litoshe kukuonyesha kuwa Yesu siyo Mungu bali ni Aliyetumwa na Mungu

Sasa nikwambie kitu?- Huwa hakuna Mungu asiye na mamlaka kamili, ukishakuwa na baadhi ya mamlaka basi wewe si Mungu
 
Na pia kwa haraka haraka unaweza ukasema Merikizedeck ndio baba wa yesu.
 
Kwa hiyo unamaanisha kuna raia zinapoteza muda kukesha makanisani na kushinda misikitini bila kujua kuwa huo ufalme hauwahusu?
 
Eliya inasemekana alienda mbinguni na usafiri kabisa wa gari ya moto. Hapa pia napata maswali mengi kuwa huko mbinguni kuna parking ya magari pia au hilo nalo ni fumbo la mwandishi?
 
Kweli kabisa Yesu siyo mungu
Ila Yesu ni Mungu
Yani mimi katika kitu ambacho siwezi kukielewa ni yesu kuwa mungu ili uamini hiki inabidi ujitoe akili na usiulize chochote nakubaliana na wewe 100 yesu sio mungu.
 
Melikzedek ni mmoja Kati ya " brothers" wanao heshimika sana in freemasonry.
 
Sawa nimekuelewa!!
Pengine,unadhani Yesu angetaja siku na majira na saa ya kuja kwake.

Ule usiri wa ile siku usingekuwepo tena
 
Kwa hiyo unamaanisha kuna raia zinapoteza muda kukesha makanisani na kushinda misikitini bila kujua kuwa huo ufalme hauwahusu?
Hapo Yesu alimaanisha kwa watakaomuamini na kumfuata (John 1:12) ndio wataelewa hayo mafumbo yake sababu watajazwa Roho mtakatifu anayejua kila kitu mpaka siri/Mafumbo ya Mungu Baba (1 Cor 2:10).
Na hii principle ipo kote mkuu hasa mashirika ya kijasusi hawawezi ongea lugha ambayo raia wa kawaida utaelewa hasa inapokua wanajadili siri za uwanja wa vita utaona tu codes nyingi hadi utachanganyikiwa.

So ukitaka kuzijua itakubidi ujiunge nao ili uweze kuwa na access na taarifa hizo hakuna namna nyingine
 

Huyo roho mtakatifu anabadirikabadirika?

Kama analeta meseji ya aina moja ya wokovu kwa kila mwenye nae mbona kuna madhehebu nyingi tofauti tofauti na hazikubaliani kwenye mambo kadha wa kadha?. Kwa mfano Biblia ya Wakatoliki in vitabu 73, Biblia ya Protestant in vitabu 66, Biblia ya Ethiopia orthodox church ina vitabu 81

Kama roho Mtakatifu ni yuleyule mmoja, na meseji ni ileile moja kutoka kwake kwa nini awafunulie watu kuwa na biblia zenye idadi ya vitabu tofautitofauti?
 
Jamaa una ufinyu sanaa wa maarifa ya Neno la Mungu hususani (Biblia)

Naomba ukitaka kujadili habari za Ufalme wa Kristo toka kwenye hali ya ushindani na ubishani,kubali kufundishika!!

Ni hayo tu
 
Jamaa una ufinyu sanaa wa maarifa ya Neno la Mungu hususani (Biblia)

Naomba ukitaka kujadili habari za Ufalme wa Kristo toka kwenye hali ya ushindani na ubishani,kubali kufundishika!!

Ni hayo tu

Nafasi ya kufundisha unayo!.
Nasubiri ufundishe!
Fundisha tu ndugu yangu tupate faida!

Sibishani naweka hoja zangu mezani, unaweza usizipende, unaweza ukazidharau, unaweza ukazipuuza lakini nitaweka tu maana hicho ndicho ninachokijua, nitafanyaje sasa au unataka kuniziba mdomo?
JF Where we dare talk openly!
 
Mkuu hii mada ni pana kidogo na nlishaijadili huku na great thinkers walitiririka naona kama una querry basi ipitie ujue wapi tofauti ilipoanza. Humu tutahama mjadala

 
kinach
kinachonishangaza ni picha yake hiyo ni wazi inathibitisha kuwa waisraeli halisi ni weusi 'tiiiii'
 

Msingi wa hoja yangu ni kukataa kumsingizia roho mtakatifu kwamba wasioelewa jambo basi hawana huyo roho mtakatifu, huenda kuna wasioelewa kwa sababu "wanafalsafa" wamewachanganyachanganya kwa falsafa zao badala ya ukweli ulio wazi na ulio simple kabisa aliofundisha Yesu Kristo wa Nazareti
 
Okay basi naomba unisaidie Yesu anaposema ametumia mafumbo (Parables) ili "kuficha" alimaanisha nni?? Je ili uweze unlock hizo siri ufanyeje??

Huo mstari unasema Roho mtakatifu anafahamu kila kitu hivyo hata hizo parables cjui unabii, ndoto utaweza zitegua ukimshirikisha maana sio kila kitu kimeandikwa kwenye Biblia.

Hakuna mwanafalsafa anayepotosha, bali kwa mujibu wa Biblia Lucifer ndio anayepotosha Ufunuo 12:9,18:2 hivyo njia pekee ya kuepuka kudanganywa ni kupima hiyo Roho/fundisho kama limetoka kwa Mungu au shetani 1 Peter 4:1-8.

Ni hayo tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…