Melchizedek na utata unaomzunguka

Kwa ushahidi upi? Yesu ni uzao wa Abraham, (Mariamu ni uzao wa Abraham ila Wayahudi wanachukua uzao kwa baba, hii ndio moja ya sababu Wayahudi hawamtambui Yesu) sasa huyu alikuwepo kabla ya uzao rasmi wa Israil jambo ambalo linaenda kinyume na utabiri, au vipi ? Naomba elimu.
 
Aiseee hii post imetosheleza kuwa thread kabisa.

Long live JF
 

Ni kweli lakin.kawa zama za kwetu ila zama ile alikua huyu melkizedeki
 
Hakuna mtu ambaye hajakutana na mbegu za kiume akawa mama ,mama ni hadhi anayopewa mwanamke ambaye gumbolake limetunza mbegu ya mwanaume tuu ikiwa ya jini au asie mwanaume huyo sio mama
 
Mada Nzuri sana.
Big up kwa wote mlioshiriki kikamilifu kabisa.
Mada kama hizi hazitakiwi kuchangiwa kwa mihemuko ya Kidini.
Nimechelewa kuiona hii mada na kutoa mchango wangu.
 
Kama Mkufunzi mose, ametia mguu katika hii mada.
Basi viwango vya hii mada vimekuwa vya juu sana.
Karibu sana mheshimiwa mose, katika michango ya mada zetu zile zenye mashiko.
Uwepo wako utatupatia maarifa mengi ya Hekima zako nyingi ulizojaliwa na Mungu Mwenye Enzi.
Nimefurahi sana kusikia kutoka kwako.
 
Maisha ya Wairani ni ya kikuani, maana kuna rais ambaye ni mtawala, alafu kuna Ayatolah ambaye kwao ni kama kuhani mkuu, uenda Salem ilikuwa Iran. Anyway dunia imeinama, mifumo imekengeuka, hakuna cha kuhani wala kuwadi, wote ni ubatili mtupu.
 
Mwandishi wa kitabu cha Waebrania ni Paulo
 
Mwanzo 14:18
Na Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye juu sana.

Zaburi 110:4
Bwana ameapa, Wala hataghairi, Ndiwe kuhani hata milele, Kwa mfano wa Melkizedeki.

Waebrania 5:6
kama asemavyo mahali pengine, Ndiwe kuhani wa milele Kwa mfano wa Melkizedeki.

Waebrania 5:10
kisha ametajwa na Mungu kuwa kuhani mkuu kwa mfano wa Melkizedeki.

Waebrania 6:20
alimoingia Yesu kwa ajili yetu, mtangulizi wetu, amekuwa kuhani mkuu hata milele kwa mfano wa Melkizedeki.

Waebrania 7:1
Kwa maana Melkizedeki huyo, mfalme wa Salemu, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu alipokuwa akirudi katika kuwapiga hao wafalme, akambariki;

Waebrania 7:10
kwa maana alikuwa katika viuno vya baba yake, hapo Melkizedeki alipokutana naye.

Waebrania 7:11
Basi, kama ukamilifu ulikuwapo kwa ukuhani wa Lawi; (maana watu wale waliipata sheria kwa huo); kulikuwa na haja gani tena ya kuhani mwingine ainuke, kwa mfano wa Melkizedeki, wala asihesabiwe kwa mfano wa Haruni?

Waebrania 7:15
Tena hayo tusemayo ni dhahiri sana zaidi, ikiwa ametokea kuhani mwingine mithili ya Melkizedeki;

Waebrania 7:17
maana ameshuhudiwa kwamba, Wewe u kuhani milele Kwa mfano wa Melkizedeki.
 
Uzao wa mwanamke YESU
Uzao wa nyoka shetani
Melichzedeck alifananishwa na mwana wa Mungu
Yesu Ni mwana wa Mungu
 
Melchizedek alikuwa malaika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…