Melchizedek na utata unaomzunguka

Hii ngoja nikae ninifunzee
 
Book of Enoch sio kitabu rasmi cha Biblia na ni ngano tu kama kilivyo kitabu cha makabayo au cha Joshua bin sira
 
Hicho kitabu cha Enock ni kitabu feki sana.

Melchizedek ni Yesu Mwenyewe, hajawahi kuwapo mtu wa namna hiyo, Yesu alijitokeza kibinaadamu apokee zile sadaka ili Abraham aweze kubarikiwa kisawasawa.

Unamaanisha kuna uhusiano wa maneno yako na haya maneno ya Yesu mwenyewe.

Yohana 8:56
Ibrahimu, baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; naye akaiona, akafurahi.

Yohana 8:57
Basi Wayahudi wakamwambia, Wewe hujapata bado miaka hamsini, nawe umemwona Ibrahimu?

Yohana 8:58
Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko.

Yohana 8:59
Basi wakaokota mawe ili wamtupie; lakini Yesu akajificha, akatoka hekaluni.
 
Naunga mkono
 
Exactly.
 
Nazani kwangu umefunga maada
 
Kwa hivi, mambo ya Melkizedek--Mwanamfalme wa Amani, Mtu wa Nyakati hata Nyakati, na tena kusema yeye ashinda katika uwanja wa vita kwa makarama ya akili na si lazima silaha; ni mambo ya maarifa na ujuzi katika ELIMU 1.0, ELIMU 2.0 na ELIMU 3.0

Yapo hata kwenye muktadha wa hili Taifa la Tanzania; 'zitazame alama'--utaanza kubaini.

 
umeishatoa jibu
 
Kwanza kabla ya kumtafuta Melkizedeki ni lazima kwanza uanze na kujiuliza namna Mungu anavyojiwakilisha na kujitambulisha kwa viumbe na ni lugha ya namna gani anatumia kueleweka kwa mzao wa Adamu.
Katika biblia tunaona sura na vifungu vya mistari katika uandishi. Lakini havikuwepo katika maneno ya nabii anaehusika na kitabu. Yeye alipokea tu neno na kulinena.
Hivyo basi elewa kuwa kazi hii ya kuweka mistari, aya na sura ni kazi ya jopo la watu waliokaa na kujadili.
Hata haya maagano mawili katika biblia yaani la kale na jipya ni wazo la jopo la waandishi. Ndani ya biblia kuna maagano mengi na mahsusi kwa mtu au makundi husika. Mfano Adamu alikuwa na agano la sheria ya kutokula tunda ambalo lilimshinda, Abrahamu alikuwa na agano la neema, kwa sababu ya imani hakuhesabiwa kosa lolote.
Mussa na watu wake walikuwa na agano la sheria
katika agano linaloitwa jipya kuna maagano pia yaani kuna kundi la ufufuo wa kwanza na wapili la watakao ingia katika harusi ya mwanakondoo na watakaorithi uzima bila kuingia harusini.
Sasa tukija kwa Melkizedeki anaonekana ni mtu wa kimiujiza maana ameelezewa kuwa hana baba wala mama wala mwanzo wa siku zake wala mwisho.
Huyu sii mwingine ila Mungu mwenyewe.
kuna aina tatu za miili ambazo ni mwili wa kiroho(teofani) miili ya nyama na damu(flesh) na miili iliyotukuzwa(ufufuko).
Melkizedeki ni mungu alishuka kumlaki Abraham katika ule mwili wa Kiroho(teofani au logos) kutoka katika mji wa Salemu(Amani au yerusalemu ya mbinguni).
Yesu alifananishwa na mfano wa melkizedeki maana yeye ni mwana. kwa kuwa Mungu yule roho alivaa mwili wa nyama na damu kutoka kwa Mariam.
mwili huu wa nyama na damu una mwanzo wake na pia una mwisho wake , una mama na baba aliyeuumba kwa kuwa haukujiumba lakini ile roho ndani ya mwili wa mwana ni ile ya melkizedeki haina baba wala mama ,,mwanzo wake au mwisho wake.
ukiyachunguza maandiko vizuri suala la uana wa mungu sii la eternity bali la kipindi cha wakati na ukuhani nao sii wa eternal bali wa kipindi cha wakati.
swala la fumbo katika Uungu ni mwingiliano wa ubaba na uana.
uana ni ule mwili wa flesh mungu aliojiumbia kwa kupitia mariamu na ubaba ni ile roho(teofani) aliyokuwepo ndani ya ile flesh.
Ule mwili wa uana utakoma hapo kazi ya ukuhani(upatanisho) itakapo koma na kurudi tena kwenye umilele(eternity).
 
Ndio Yesu mwenyewe mkuu. HIV mambo ni za kiroho sana kuzielewa.
 
Melkizedeck alikiwa ni Mungu mwenyewe
Hana baba hana mama.
Hana mwanzo wa siku zake wala mwisho wa siku zake
Mfalme wa amani
Waebrania 7 inaelezea
Alipokea fungu la kumi la ibrahim akapotea pasipojulikana.
 
DR Mambo Jambo
Rabbon
 
Ufalme wa Melkizedeki ulishapita kabla hata taifa la Israel halijawepo, kwanini useme awe mtawala wa race inayokuja ?
 
Ufalme wa Melkizedeki ulishapita kabla hata taifa la Israel halijawepo, kwanini useme awe mtawala wa race inayokuja ?
Waebrania 7:2-3

"Ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, tena, mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani;

To whom also Abraham gave a tenth part of all; first being by interpretation King of righteousness, and after that also King of Salem, which is, King of peace;

hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu);
huyo adumu kuhani milele.

Without father, without mother, without descent, having neither beginning of days, nor end of life; but made like unto the Son of God;
abideth a priest continually."


Zingatia Neno Abideth A priest Continually..
na hapo Ni Kitabh cha waebrania Agano Jipya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…