Melchizedek na utata unaomzunguka


Kwa nini usidhani kuwa Melkizedeki ni FATHER na siyo SON( yaani Yesu)?

Au na wewe unadhani kuwa FATHER ndiyo huyohuyo SON (Yaani Jesus)?
 
Mkuu kumbe upo vzuri hadi sekta za Imani..... Indeed you are a great thinker.
 
Kwa nini usidhani kuwa Melkizedeki ni FATHER na siyo SON( yaani Yesu)?

Au na wewe unadhani kuwa FATHER ndiyo huyohuyo SON (Yaani Jesus)?
Mkuu ni wapi nimesema melchizedek ni Yesu/Mungu??
Wapi nmeongelea Yesu na Mungu kuwa kitu kimoja?? Hizi assumptions unatoa wapi??

Stick kwenye mada
 
Inaonekana figurative language ya Bible ni changamoto!! soma 1 Peter 1:23 alafu uniambie umeelewa nini??

Ukimaliza gusia Mathew 12:47-50

Then Ufunuo 14:4

Nataka upate connection ya seed,birth and Baba figuratively
 
1. Labda niulize, ni wakati gani biblia ni figurative na wakati gani bible ni Lateral??

2. Agano la kale lote linamtabiri Kristo na hata hao wayahudi ndio waliofanya hivyo ukisoma new testament imejaa citations za unabii wa Agano la kale juu ya Yesu.

3. Bible inasema melchizedek hakua na baba wala mama je wapi wamesema alikua na ukoo??

4. Book of Enock inadai hakuzaliwa na mama wala Baba sasa wapi atoe ukoo?

5. Hakuna anayetumia akili zake bali wanakusanya dots mfano sifa anazopewa melchizedek anapewa Yesu ndio maana wanajaribu kuweka ulinganisho.
Ni sawa na Yule mtoto wa Ufunuo 12 au Mpanda farasi mweupe wa Ufunuo 6 na 19?? Hajaitwa Yesu ila sifa alizopewa ni za Yesu pekee.
 
Agano la kale ni kivuli cha Agano jipya. Maana yake yaliyotokea yaliakisi yatakayotokea katika Agano jipya. Mzee Mwanakijiji kaandika vema nami naandika kwa kiasi.

Tuanze na Yohana 8 ambapo Yesu alikuwa akijibizana na mafarisayo kuhusu Yeye ni nani:

Yohana 8
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁵⁶ Ibrahimu, baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; naye akaiona, akafurahi.
⁵⁷ Basi Wayahudi wakamwambia, Wewe hujapata bado miaka hamsini, nawe umemwona Ibrahimu?
⁵⁸ Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko.


Hapa Yesu anatupa dokezo kuwa kuna mahali wakati Ibrahimu akiishi hapa duniani walikutana hivyo basi tukitafuta kwenye Agano la kale tutakuta mahali fulani habari ya Yesu na Ibrahimu. Twende kwenye Agano la kale:

Mwanzo 14
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁸ Na Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye juu sana.
¹⁹ Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi.
²⁰ Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote.


Hapa kuna mambo matatu muhimu kumhusu Melkizedeki:
1. Alikuwa mfalme wa Salem
2. Alileta mkate na divai wakala pamoja
3. Alikuwa kuhani wa Mungu aliye juu

Ikumbukwe kuwa katika Biblia yote hakuna mwanadamu aliyetajwa kuwa mfalme na kuhani kwa wakakati mmoja isipokuwa masihi tu. Tuone andiko moja tu kwa mfano:

Zekaria 6
¹³ Naam, yeye atalijenga hekalu la Bwana; naye atauchukua huo utukufu; ataketi akimiliki katika kiti chake cha enzi; na kutakuwa na kuhani katika kiti chake cha enzi; na shauri la amani litakuwa kati ya hao wawili.


Ok, tukiangalia hayo mambo matatu, salem (shalem kwa kiebrania) sio mahali, bali ni ufafanuzi. Maana yake ni amani, hivyo alikuwa mfalme wa AMANI, sifa ambayo imetajwa kuwa nayo masihi pekee.

Isaya 9
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁶ Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani.


Alileta mkate na divai ambayo ni komunyo. Angalia jambo hilo lilifanyika pia kwenye Agano jipya.

Tuangalie sasa Waebrania:

Waebrania 7
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹ Kwa maana Melkizedeki huyo, mfalme wa Salemu, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu alipokuwa akirudi katika kuwapiga hao wafalme, akambariki;
² ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, tena, mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani;


Kumbe hata neno Melkizedeki sio jina kama tulivyodhania, ni maelezo tu. Melkizedeki = mfalme wa haki. Yesu ndiye atakayehukumu kwa haki, yeye ni mfalme wa haki pia mfalme wa amani.

³ hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele.


Nadhani umeona parallel iliyopo kati ya Agano la kale na jipya, hicho ndicho kivuli kilichokuja kudhihirika kwa Agano jipya.

Kama hujaelewa uliza.
 
Nikajua wewe ni mtaalam wa uchambuzi wa Siasa kumbe uko vizuri sana hata kwenye maswala ya maandiko. Umeelezea vizuri sana
 
Hizi ngonjera ndio waga nazikata, kwaiyo wakiandika "Yesu akaenda Galilaya" ukitumia akili zisizo za kimamalia kama usemavyo ndio itasomeka Yesu akaenda msumbiji au....!!!? Tusichoshane[emoji124][emoji124][emoji124]
Inasemekana ya kwamba kuwaelewa waandikaji wa biblia hupaswi kutumia akili za kimamalia
 
Kunawatu mko deep yani unaelezea hadi unauona utukufu unashuka na kukufunika. Barikiwa
 
Hizi ngonjera ndio waga nazikata, kwaiyo wakiandika "Yesu akaenda Galilaya" ukitumia akili zisizo za kimamalia kama usemavyo ndio itasomeka Yesu akaenda msumbiji au....!!!? Tusichoshane[emoji124][emoji124][emoji124]
🤣 🤣🤣
 
Ivi kwa nini lakini hawa waandishi walitumia lugha ya mafumboo..!!??
Vichwa panzi hapa unatoka kapaaa...!!

But why?...Whyyy??
Kusoma neno la Mungu hadi uelewe inahitaji uombe kwanza roho mtakatifu afungue fahamu zako

Hata wale wanafunzi wa Yesu kuna mda walikua hamwelew wakamwomba awatafsirie
 
Mkuu naona ww na Mzee Mwanakijiji mmetegua hiki kitendawili.

Ubarikiwe sana mkuu.
 
Kudos[emoji122].ufafanuzi mzuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…