Meli inayosimama dede baharini

Meli inayosimama dede baharini

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Chombo cha utafiti RV Flip ndicho chombo pekee duniani chenye uwezo wa kuhama kutoka mlalo wa kuelea baharini hadi uwezo wa kusimama wima katikati ya bahari.

Flip sio meli ndogo, ina urefu wa mita 108 na uzani wa tani 700. Wahandisi waliitengeneza ili iweze kusimama wima.. Sema dede kwenye nyuzi 90 iliyonyooka, na sehemu ya mbele ya meli iliyo juu yenye na urefu wa mita 17 (yaani jengo la ghorofa 5 kwenda juu) huku chini ikiwa imezama kwa urefu wa mita 91.

Yaani meli nyingi zimezama chini ya maji kwa urefu huo. Teknolojia na uhandisi uliotumika husaidia utulivu wa meli na upinzani dhidi ya mawimbi, mchakato wa mabadiliko huchukua wa kuifanya isimame dede huchukua muda wa dakika 30, ambapo maji ya bahari hupigwa ndani ya matangi makubwa nyuma ya meli, ambayo huifanya kuzama ndani ya maji na kuifanya meli kuwa katika mwonekano wa wima.

Meli hii inachukuliwa kuwa miongoni mwa meli muhimu sana katika nyanja ya utafiti wa kisayansi wa bahari.

FB_IMG_1727153153271.jpg
 
kaka mkubwa unaongelea meli kweli au? mana we bwana kwa tafsida ujambo usikute hapo unaiongelea ccm na mb owe ooh kumbe umeweka na picha hapo kidogo naanza kuamin kwa mbali hata hvy ngoja niendelee kusoma coment mana hukawii kutupiga kiin macho usikute hiyo meli mkia wa nyum ccm ndio inazama alafu huko mbele chadem mana nyie walonz mnatabia ngumu sana
 
Back
Top Bottom