3 May 2021
Matema Beach,
Tanzania
MELI ZA TANZANIA ZAKUMBWA NA DHORUBA KALI KTK ZIWA NYASA
Kutoka Ziwa Nyasa meli mbili zinazomilikiwa na Mamlaka ya Bandari ya Tanzania zimekumbana na dhoruba kali inayoambatana na mvua kubwa.
Meli ya abiria MV Mbeya II imepigwa na mawimbi makali jioni hii huku ikiwa na abiria 87, maofisa na mabaharia 25 na kusukumwa mpaka Pwani na kukwama. Uwezo wa meli ya MV Mbeya II ni abiria 200 na mizigo tani 200.
Meli hii MV Mbeya II yenye mitambo ya kisasa kama echosounder, GPS, Radar , magnetic compass, spidi 11 knots na ni meli aina ya landing craft inayoweza pia kushusha mizigo na abiria popote kusipokuwepo na gati.
Meli nyingine ndogo ya mizigo MV Songea pia inayomilikiwa na Mamlaka ya Bandari ya Tanzania TPA imekumbwa na mawimbi makubwa makali muda wa mchana na kunasa ktk pwani ya mchanga (fungu) kutokana na hali mbaya ya hewa yenye upepo mkali na mawimbi makubwa.
Mkuu wa wilaya Kyela nchini Tanzania na kamati yake ya ulinzi na usalama,wamethibitisha kadhia hiyo iliyozikumba meli hizo mbili zinazotoa huduma katika ziwa Nyasa.
Meli ya MV Mbeya II ilizinduliwa mapema mwezi Januari mwaka huu 2021 kuanza safari ktk ziwa Nyasa WAZIRI MKUU azindua meli mpya ya abiria ya MV Mbeya II katika ziwa Nyasa
Source : millard ayo
N.B
Utabiri hali ya hewa
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania tarehe 3 May 2021
Source : meteo tanzania

Jamvi online tv Meli ya MV Mbeya II inaudwa baada ya meli ya mwanzo ya MV Mbeya I kuzama mwaka 1975 eneo la Makonde wakati ilipokuwa ikifanya safari zake za kawaida katika ziwa hilo. Source : UJENZI WA MELI MPYA YA ABIRIA MV MBEYA II KATIKA ZIWA NYASA WAFIKIA ASILIMIA 82, AWAMU YA TANO NI VITENDO TU | Full Shangwe Blog