DOKEZO Meli ya MV. Victoria (Mwanza) haina crane ya kubebea mizigo zaidi ya miezi miwili, ni hujuma?

DOKEZO Meli ya MV. Victoria (Mwanza) haina crane ya kubebea mizigo zaidi ya miezi miwili, ni hujuma?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

NBica

Member
Joined
Sep 13, 2010
Posts
39
Reaction score
36
WhatsApp Image 2024-11-06 at 08.08.12.jpeg

Meli ya MV. Victoria iliyo chini ya Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) inayofanya safari zake kati ya Mwanza na Bukoba, kwa miezi kadhaa sasa “crane machine” haifanyi kazi baada ya kuharibika.

Hatua hiyo kwa namna moja au nyingine inaikosesha Serikali mapato yatokanayo na shehena ya mizigo kutoka au kuingia kwenye mikoa husika na mingine ambayo inatumia njia ya Meli kusafirisha mizigo mizito.

Hali ilivyo sasa, Wananchi wanaotaka kusafirisha mizigo yao wanalazimika kuwalipa vibarua kwaajili ya kupakia au kupakua mizigo ndani ya meli hiyo huku wengine wakirejea kwenye usafiri wa fuso na malori.

Je, ni kweli MSCL hawana hela ya kutengeneza mashine hiyo au wanachukulia poa?

Tetesi zilizopo ni kuwa inadaiwa kuna hujuma fulani inaendelea ambapo kuna Watu hawataki crane hiyo tengenezwe ili ile mizigo mizito isafirishwe kwa njia ya Barabara.

Pia soma - MSCL: Ni kweli mtambo wa kubebea mizigo wa MV Victoria ulipata hitilafu ya kiufundi
 
Back
Top Bottom