Kwa bahati mbaya
Red Giant alileta picha hizo kiholela bila kutaja vyanzo alikozipata (fujo ya kawaida hapa JF)
Ila tu kimsingi ni kweli tunaweza kuangalia mabaki ya mashua ya kale kwenye makumbusho hapa na pale. Maana kama kitu cha ubao kilizama kwenye maji na kufunikwa kwa matope hali kwamba wala wadudu wala oksijeni ya hewa inaweza kufika, na baadaye maji yamekauka, au mto umebadilika njia yake, basi kitu kile kinahifadhiwa chini ya ardhi.
Wakati wa kujenga nyumba kubwa au barabara siku hizi wanaweza kukuta kitu kile, wasipoiharibu lakini kutambua ni kitu cha kale na kuita wataalamu kinaweza kutolewa. Baadaye kuna kazi ya kuihifadhi, hapo wako wataalamu wengine, halafu inaweza kuonyeshwa kwa umma na kufanyiwa utafiti na wataalamu wengine tena.
Mfano boti inaweza kutufundisha kuhusu ufundi wa kale, nyenzo walizotumia, aina ya miti na kadhalika. Vivyo hivyo maiti, vyenzo, mabaki ya nyumba, vyungu (rahisi zaidi kutunza) hadi kuchungulia mabaki ya takataka (kama imehifadhiwa) je walikula chakula gani?
Kupima umri inawezekana kwa mbinu mbalimbali, pamoja na C14