Mema na mabaya ya mabeberu

Mema na mabaya ya mabeberu

GIRITA

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2016
Posts
4,432
Reaction score
5,864
Habari,

Niwape pole kwa mapambano makubwa ya kujiepusha na athari zinazotokana na ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na virusi vya corona.

Moja kwa moja tuangalie mambo yanayofanywa na jamii ya wazungu kama tunavyofaham,iwe ni Wa kutoka bara LA america au ulaya.

Jamii hii na mataifa yao imekuwa na nguvu kubwa ya kiuchumi mpaka kuwa tegemeo kwa mataifa yasiyo jiweza hasa katika bara letu la Afrika. Yafuatayo ni mambo aina mbili wanayofanya kwa waafrika:

Mema:
~ mikopo ya kifedha.

~ huduma za kiafya.

~ misaada ya kielimu.

~ misaada kupitia taasisi za kidini.

~ misaada ya pembejeo za kilimo.

~ misaada katika sekta utamaduni na utallii.

~ misaada ya miongozo katika siasa.

~ ujenzi Wa miundo mbinu.

~ kuhudumia makambi ya wakimbizi na kuwapeleka katika nchi zao kuishi.

mabaya
~ kupora Mali za waafrika na kujinufaisha kwazo.

~ kudhamini makundi ya waasi na kuvuruga amani.

~ kugeuza afrika kama shamba LA bibi kufanyia tafiti za madawa wanayoyagundua.

~ kukontroo serikali zetu kwa kutupangia cha kufanya.

~ kuwapoteza viongozi wenye misimamo wanaopingana nao.

~ kuandaa viongozi vibaraka kuwapa madaraka kwa ajili ya manufaa yao.

~ kuwabagua waafrika wanapokuwa wanaishi katika nchi zao.

~ kuingia mikataba ya kinyonyaji kwa ajili ya maslahi yao binafsi.

Yapo mengi mema na mabaya ambayo yanafanywa na watu hawa, binafsi tumewahi saidiwa na mzungu mmoja...tulikuwa tumeenda kucheza mechi ya Mpira Wa miguu hatukuwa na jezi...akatupa SETI ya jezi pea NNE na mipira mitatu bila kumuomba.

Jamaa alikuwa na moyo Wa kutoa, kumbe allikua na kontena zima LA vifaa vya michezo, kwa ajili ya kusaidia vijana Wa kiafrika..alikuwa mchezaji Wa Blackburn rovers ya england miaka ya 2005.

Watu wengi wamekuwa wakilalamikia mabeberu kwa vitendo vyao viovu kwa afrika,lakini pia hawa viumbe wana utu na unyama hivyo tuishi nao kwa Tahadhari ikibidi kuachana tuachane kwa Tahadhari.
 
~ mabeberu in da house!!
 
Nachukia sana tabia ya kuwaita hao jamaa mabeberu, kwahiyo sisi mbuzi jike au?
 
Ukitaka kumtawala mtu mnyime elimu. Asilmia kubwa bado hawana elimu ya kutosha.
 
Elimu yenyewe ni yao...hapo ndio tatizo,huwezi kuwa zaidi ya alikuletea hiyo elimu.
Ukitaka kumtawala mtu mnyime elimu. Asilmia kubwa bado hawana elimu ya kutosha.
 
Back
Top Bottom