Memba Mpya

massa danata

New Member
Joined
Mar 11, 2018
Posts
1
Reaction score
3
Nawashukuru kwa kuniruhusu kushiriki nanyi humu. Nimekuwa mgeni fiche kwa miaka mingi, na ni leo nilipopata ujasiri wa kujisajilisha.

Haja yangu haswa ni kuimarisha kiSwahili changu. Huenda nitabarikiwa kupata watoto miaka inayokuja na ninatamani sana kuwafunza kiSwahili ili wao pia na waweze kuwafunza wanao. Lakini pia najitolea kuwasaidia wenzangu wowote wanaohitaji msaada na Kiingereza, na ninaweza kujaribu pia ikiwa kuna yeyote atakayetaka usaidizi na Kiespania au Kijerumani.

Mimi najitambulisha kama Muafrika Mashariki na ninaimani kuwa uhusiano wetu nchi hii / eneo hili utaendeshwa na uchukuzi wa tamaduni tunazozibuni pamoja (kwa kiingereza cultural exchange). Ninavutiwa sana na ustadi wa utungaji wa mashairi na nyimbo, nikiamini kuwa ubuni huu una. Mimi ni mzaliwa wa Nairobi ila sipendi kamwe kiSwahili kibovu cha huku. Huwa nakereka sana nikiwaona wazazi wakiwafunza wanao kiSwahili kibovu, na ninahofia lugha yetu itafifia. Sipendi pia kuwa kiSwahili changu ni duni sana nikilinganisha na kiingereza changu. Ninapokutana na mPwani huwa naona aibu sana kutojua lugha yetu. Kweli, nakiri kuwa lugha sio kumbikumbi ila inaendelea ikibadilka na mikopo ya maneno na mabadiliko ya kimaana na kimatamshi. Lakini natamani uhifadhi fulani wa desturi / kanuni za kilugha.

Yangu yatakuwa maswali kuhusu misamiati, hususan maneno ambayo siyapati mtandaoni, kwenye kamusi, au matumizi ambayo ni kinyume na nilivyotarajia.

Shukran kwenu
 
Kalibu sana jf kila mtu huku ni great thinker,pia kila mtu anamaisha bora,pia kila mtu anamiliki usafiri
 
Karibu jf ndugu jiskie huru namwenye bahat pia kua hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…