Membe amwaga siri Hayati Magufuli alivyomfitini na kumkosesha Ukatibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola

Haya anayosema Membe yanaweza kuwa ya kweli au uongo ukizingatia anayasema wakati upande wa pili haupo.
"MAREHEMU asemwi mtu ukifa kitabu chako kimefungwa"
Tusingesoma historia Bro, tumwache ateme nyongo zake ni haki yake kikatiba bro tumvulie kila mmoja wetu. Kuna cha kujifunza hapo. Hatuwezi kuyafukia haya ukweli uwekwe tu peupe kwa faida ya vizazi vijavyo, they should not repeat the same mistakes bro.
 
Atakayeing'oa CCM madarakani ni mwana CCM. Sisi tutaendelea kuwa ndugu watazamaji.
 
Ni Afrika na hasa Tanzania vilaza wanapokuwa kwenye orodha ya kugombea nafasi nyeti kama urais.

Huyu tumemuona kwenye wizara ya mambo ya nje ni kiazi fulani hivi hata huko TISS kama kweli alikuwepo walipata hasara sana.
Tunafahamu wote kuwa Mtumishi wa TISS haruhusiwi kujitaja kama kuwa yeye ni TISS (isipokuwa 'DG' pekee ndiye anayefahamika tena na yeye binafsi hajawahi kujitaja ila sababu ya nafasi yake ndiyo imepelekea afahamike) anavyofanya huyu Maembe .

Halafu, anayoyasema hajui kuwa yanaiweka Tanzania na nchi zingine alizozitaja kwenye taharuki fulani fulani, mfanyakazi wa TISS, mwanadiplomasia hajui kuwa aliyoyasema ni tatizo!?

Huyu anayeijiita 'kachero mbobezi' hajui kusema kuhusu pesa za Jumuiya ya Madola, anaonekana ni mpenda pesa na mbadhilifu!?

Hafahamu kabisa kuwa, kutaja kuhusu Rais Samia, anaweka mpambano kuwa mkali 2025?

Halafu, umpe huyu hata uwaziri wa wizara yoyote tambua hiyo inakuwa ni hasara kubwa kwa nchi.
Wale wanaoishi huko jimboni kwa Maembe, watujulishe kwa muda wake wote kama Mbunge alifanya nini cha maana!? Hii itatusaidia kupima uwezo wa hawa wanasiasa kupewa nafasi ya urais.
Mwingine karejeshwa wizarani lakini sijui cha maana alichokifanyia Tanzania na jimbo lake kwa miaka yote hiyo 15+ hata akarudishwa tena kapewa wizara nyeti ya nishati!?A u Tanzania imekuwa kwamba, katika nchi ya vipofu chongo ndiye huwa mfalme!?

Tanzania, tunaendelea kupigwa kwa kweli.
 
Inchi hii ngumu sana, anamsema mwenzake kua raisi wa MiundoMbinu while yy muda wote anazungumzia mahusiano ya kimataifa...kweli Nyani hajawahi ona Kundule...[emoji1787][emoji1787]
Yeye si raisi.
 
Hapa hukumuelewa ndugu Crimea. Alijaribu kuhoji kwamba ni nani alifungwa kutokana na haya mauaji. Maana yake ni kwamba anathibitisha haya yalifanywa na awamu ya JK na hakuna alichofanya. In short tawala za viongozi wote zimejaa damu za watu. Watalizipia kwenye makaburi yao.
 
Ok zile 7b zimempita na kaongea machungu yote na alivyofanyiwa
Kwa hiyo sasa anaomba kama nafasi nyingine ikitokea apitishwe na mama au

Maana anaeleza kuwa hatagombea Urais na atamuunga mkono Mama

Haya yetu macho na matatizo duniani yameongezeka na dau pialimeongezeka naona litakuwa 10b kwa sasa
Amesema huwa wanachagua kila baada ya miaka mingapi vile

Naona yuko mkao wa kula masikini kina mama kwani hela zinatolewa kwa ajili yao ila hawapati hata senti

Mungu tusaidie kwani kuna watu wengine ni walafi sana na huwa wanaangalia fursa tu
 
Raisi angempromote membe kwenye hiyo nafasi na kumtakia kila la heri kwenye majukumu yake mapya kisha kumpa angalizo la kutokuipaka matope nchi angepoteza nini zaidi ya kuimarisha uhusiano?
 
Mkuu umelisoma hilo eeh,
 
Hypocrite.
 
Upande wa pili wa hii hadithi unaonyesha roho ya kutopenda kuona mtanzania yupo juu ya JPM kicheo na kiumaarufu.

..kinachoharibu legacy ya Magufuli ni matendo ya kikatili na umwagaji damu yaliyokuwa yakiendelea ktk utawala wake. Na kwa bahati mbaya sana Magufuli hakufanya juhudi zozote zile kujitenga nayo. raisi akionekana amebariki chuki na ukatili liko kundi kubwa ambalo litamuunga mkono. Magufuli ameondoka lakini ametuachia hali ya malumbano yasiyo na tija, chuki, na kutokuaminiana, miongoni mwa Watz.
 
Baba huyu haoni aibu kusema haya hadharani? Anaona ufahari kuwa dalali wa nchi yake kwa faida yake binafsi?

Wonders shall never end in this world!

Hii ni yeye kasema au wanamsemea? Mbona hapo JPM anaonekana mzalendo zaidi kwakumzibia hiyo nafasi?

Unawezaje kutamani nafasi ambayo kiongozi wako wa nchi atakuwa hana fellowship nayo? Kwa faida ya nani ili iweje? Unaweza mchukia JPM kama indivifual, lakini tunasahau sisi wengine hatumwoni JPM person tunamwona JPM Rais....Hapa ndipo watu wetu wanafikiriaga in opposite direction...Tunashindwa kutofautisha cheo cha mtu na personality yake...Kama alishindwa ku negotiate na Rais wake definately anayo weakness mahala na hawezi tofautisha issues with personalities...
 
Upande wa pili wa hii hadithi unaonyesha roho ya kutopenda kuona mtanzania yupo juu ya JPM kicheo na kiumaarufu.
Kwanini usiwaze kwamba alikuwa hataki atumiwe kuhujumu taifa letu wenyewe kwa kipande cha pesa?

Umeelewa maelezo yake lakini? Kama bado hizo pesa kazi yake ni ipi na thamani yake ukilinganisha na watakayochukua kupitia hiyo diplomasia?

Kwanini unadhani hawakunichagua mimi au wewe? Can't you see what was needed from him? Ebu tuweni basi na critical analysis japo kidogo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…