Membe amwaga siri Hayati Magufuli alivyomfitini na kumkosesha Ukatibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola

Hizo porojo za huyu bwana hakuna wa kuziverify, naye kajaa chuki tu.
 
Yawezekana kweli mwendazake alikuwa na dosari zake,Lakini Membe naye ni wazi ni empty set na ama makandokando mengi pia.

Na imani sasa anatamani kurudi ndani ya CCM ila anakuja na style ya kutafuta HURUMA YA UMMA. ebu jiulize mtu unaanza kuongea vitu vya zamani ambavyo hata unayemshutumu hana uwezo wa kukujibu kwa sasa ,maana ni marehemu tayari, anayaongea leo sisi wananchi tufanyaje,?Tumsaidiaje?
Anatafuta Huruma ili arudi kwa kishindo CCM,bila shaka hajakata tamaa na urais.
 
Angeenda kutuaibisha kama mama yenu.
Maana juzi tumemsikia alisema Tanzania imeathirika na mabadiliko ya Tabia ya nchi
 

..madai mengine ya Membe ni kwamba Magufuli alikuwa na upeo mdogo sana kulinganisha na madaraka ya Raisi.

..ndio maana akamlinganisha na nyuki mwenye kutengeneza asali tu, lakini hawezi kutengeneza vitu vingine.

..Membe pia amesema Magufuli alikuwa akifanya vizuri ktk miundombinu peke yake huku mambo mengine " nyeti " akiwa hana habari nayo.

..Kwa mfano, ktk awamu ya 5 tuliboronga ktk diplomasia na mfano mzuri ni suala la Sahara Magharibi.

..Pia amelaumu Tanzania kutopeleka askari kusaidia Msumbiji ktk vita na magaidi. Kwamba Rwanda kuingia kijeshi Msumbiji kabla ya askari wetu kufika kule ni fedheha kubwa kwa Tanzania.

..Msumbiji ni ndugu zetu wa DAMU. Tuliwasaidia ktk vita vya ukombozi. Na Msumbiji walituma askari wao kutusaidia kumpiga Iddi Amin.

..Zaidi ya hayo aliyoyasema Membe mimi kwa maoni yangu naona Magufuli alikuwa very very inefficient ktk kutekeleza majukumu yake.

..Hata aliponuia kufanya jambo lenye manufaa alilitia dosari kwa maamuzi ya kukurupuka, kujiona anajua kumzidi kila mtu, lugha mbaya, na visasi.

..Chukulia mfano wa ATCL; kuna madeni ya bilion 400++; hasara ya bilion 60++ kila mwaka. Kwanini tuingie kichwakichwa kununua ndege za matrilioni toka kwa mabeberu?

..Kwanini matrillioni yaliyotumika kwenye manunuzi ya ndege hayakuelekezwa kwenye sekta au miradi isiyo na mzigo wa hasara ukilinganisha na ATCL? Kwanini hatuku-invest kwenye kilimo cha umwagiliaji? Kwanini hatuku-invest kwenye viwanda?

..Fedha nyingi alizoweza kukusanya, jambo zuri, alizitumia vibaya ktk miradi inayotia hasara, au ambayo muda wake ulikuwa haujafika. On top of that alikuwa kiongozi MKATILI, mbaguzi, na laghai.
 

Hana lolote huyu mpuuzi. Ni nani hulipiza kisasi kwa kujidhalilisha yeye mwenyewe? Hata sungura alisema, “sizitaki mbichi hizi” baada ya kurukaruka na kushindwa kuyafikia matunda kwenye mti.

Even Dr. Rungwe is politically stronger than this loony!
 
Andiko lako zuri ila ni kitabu kabisa
 
Ila haikua freshi watanzania wengi walikosa fursa kwa kuzuia Membe, huyu jama wako alikua kama shatani
Wakina Asha Migiro alikuwa Naibu katibu mkuu wa umoja wa maitafa mbona hatukuwai kuona Watanzania wakiajiliwa;hizo ajira Membe angezitoa Wapi?Membe ni mwizi tu,alizurumu ela za Gadafi na kwenda kujenga hotel ya kifahari kwao Lindi, ndio maana Magufuri alikuwa akiwapiga pini
 
Hivi hadi leo tunajua ambaye JPM alilalamika kumuwekea sumu? Mambo mengine sisi raia hatujui vingi nyuma ya pazia.

Alafu issue ya kusaidia kijeshi JPM alisema gharama ambazo tulishaingia inatosha toka uhuru! Sasa tujenge uchumi wetu! Alafu huyo Jasusi anatoa siri namna Msumbiji tunavyoshirikiana!!! Politics ambazo siku hizi hawanipati!
 
Pamoja na mapungufu ya kibinadamu ya JPM lakini kuna sehemu katuvusha na pia kuna somo tumepata. Hawa hawatotudanganya kirahisi tena na sasa hata wao hawatojiachia ovyo!
 
Kitendo cha kufungua mjadala kumsema aliyetangulia ukijua hawezi kukujibu ni uoga na unafiki uliyopitiliza, hii ni mbinu ya kujitetea tu ukifuatilia hoja zake hazina mashiko. Naanza kuhisi alibanwa, hivi sasa ndiyo anapumua.

Angekuwa ni mwanaume na mwenye uthubutu angeeleza haya kipindi mwenyewe yupo hai hata awe kajificha nchi fulani. Ila kwa uoga wake akijua angejibiwa na kuanikwa uozo wake maana JPM hakuwa akibakisha chenchi, anaongea tu ukweli wwnyewe.

Haya kaja kuropoka akiwa ni marehemu kwa kufahamu hakuna shambulizi dhidi yake, ambalo lingeweza kuharibu career yake kisiasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…