Membe amwaga siri Hayati Magufuli alivyomfitini na kumkosesha Ukatibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola

Eti Membe shushushu mbobezi kwa mujibu wa JF na Tanzania.

Ngoja niwaambie afisa usalama wa juu nchi za wenzetu, they are based on ‘Plato Republic’ Philosophy.

Ndio wanaoshikilia top civil services post makatibu wakuu, wakuregenzi wa wizara, P.A wa mawaziri, viongozi wa taasisi nyeti za serikali kama vile uhamaiji and other sensitive institutions.

Na hao watu awaokotwi tu, wengi wao wanaanza kuwa recruited soon as they finish university with top grades halafu wanaanza kuwajenga uwezo wenyewe.

Sasa hadi ufikue kuwa top senior civil servants lazima uridhishe uwezo wako zaidi maana recruits wenye uwezo kutoka uni mko wengi.

Ukiwaridhisha kupitia mchakato wao wa performance appraisal kwa nafasi unazopewa serikalini ndio unapanda mpaka juu.

Na ukifika juu unapokea mshahara mkubwa kuliko raisi wa nchi na mawaziri (senior civil servant anachozidiwa na viongozi wa nchi labda ni marupurupu tu).

Kwanini wanalipwa ivyo waache tamaa na nafasi zao mara nyingi ni permanent ili wasiwe na uoga kwenye kutetea maslahi ya taifa kwa serikali yeyote itakayo ingia madarakani.

Sasa sisi tuna usalama wa taifa wenye shutuma za kuuza unga, kuchota hela za misaada, hawana track records za mafanikio, watu wanaotetea ufisadi, wenye tamaa za madaraka; halafu JF inaita hao watu top spies.

Nyie watu kuelewa mchezo wa usalama wa taifa bado sana, ni hivi mabeberu hayana interest na nchi maskini kama Tanzania; ata hiyo gas kuna zina reserve nyingi zaidi kushinda Tanzania hadi serikali zao kuingilia kati.
 
Kumbuka ni adui mkubwa wa Kagame,PK anamtuhumu kuchukua pesa za ufaransa kusaidia waasi wa Rwanda
 
Ukimwangalia Membe jinsi alivyo .Hana uwezo hata wa kuongea.Hana ushawishi wowote.Hana mvuto wowote .Mnamwita shushu mbobezi.Anaongea kama MTU asiye na elimu yeyote.Hawa wote wanaotoka mafichoni ni wale wanafiki ,ambao masilahi yao binafsi yaliminywa na Magufuri.Sasa wanatueleza ili tuwasaidie nn?Yaan ni kikundi cha wahuni ,ambao wanafikiri watanzania bado ni wajinga.
 
Mh!! Nchi yetu inaongozwa na watu wa ajabu Sana!! Inamaana huyu ndie alikua kiongozi wa TISS?!!

Anatoka hadharani kabisa anasema alimchukia marehemu na kumpinga kwasababu alimnyima ulaji wa uongozi huko commonwealth.?!!

Haoni marehemu angekua hai angemjibu kua alikua fisadi na alimkatalia kwa maslahi mapana ya nchi.!!

Halafu kiongozi mstaafu wa TISS unalaumu Marehemu.?!

Ila point taken ni kua umethibitisha kua Serikali ya awamu ya tano, ambayo makamu wa Raisi ambaye sasa ni Raisi waliua watu.
 
Saioni kwann umnyime mtanzania mwenzako nafasi sababu unaona atakuwa fisadi. Mupe kisha kaa nae chini mueleze unalotegemea kutoka kwake.

Ni sawa na mtoto wako kafaulu ila unagoma kumlipia ada kwamba unahisi atavuta bangi huko shule halafu nafasi yake unampa mtoto wa jirani.

Hapa, pamoja na madoa ya membe ila raisi wetu hakuwa sawa.
 
Alikuwa wapi kusema haya yote!
Ndugu,
nina imani kabisa hata wewe wajua ukweli fika kuwa angejaribu kuyasema haya wakati ule uwezekano MKUBWA asingekuwa hai sasa hivi.
Pamoja na yote ambayo ni ya kwake binafsi, anachokifanya sasa hivi ni chema na chaweza HATIMAE kuja kusaidia kuisafisha nchi yetu.
Nasi kama wazalendo wa kweli twatakiwa tufurahiye na tusichoke kujifanyia tafakuri kama TAIFA, kuufukua uchafu mwingi sana uliyotutia doa ambao kuna watu bado wanashindana kuupulizia 'manukato'. AMEN
 
Haya alitakiwa ayaseme Magufuli akiwa hai,kwani hakuna sehemu kavunja Sheria.
Kinachonishangaza unafiki na kujipendekeza ,hakika anajidharaulisha, matendo yao yanajulikana wazi ,ni majizi ,matapeli, mafisadi,ambao mwendazake aliwatia adabuw haswa

Usitegemee mtu aliyewakimbia wapiga kura na chama kilichompa dhamana kugombea urais kuwa uthubutu wowote wa kuongea ukweli.
Mwache afurahishe wanakijiwe wenzie kwa kuwapa story za uongo na utapeli wake. Ila wanakijiwe na nyie jiongezeni.... membe si ntu😂😂
 
Na alisema mengi mbona. Hivi kuna mtanzania ambaye ilionekana wazi hapatani na JPM kama Membe? Yule ilikuwa wazi kabisa kuwa yeye na aliyekuwa raisi wetu hawapatani. Sema wengi waliamini kuwa Membe anataka kumnyang'anya uraisi ila kwa mwenye akili angeona kabisa kuna sababu nyingine. Pia Membe alijua kabisa chini ya ACT hawezi kuwa raisi.
 
Membe na tuhuma zoote alizonazo za uchafu, kama ni kweli raisi wetu alifanya hilo la kukata majina ya kina mula na yeye basi hakuwa sahihi.
 
Acha unafki inawauma mlishindwa kumwambia jiwe alete katiba mpya zaidi mlipiga vigelegele na kutaka kumpa mitano tena
 
Kwa hilo la kumzibia membe asee kweli jpm hakuwa fair. Lkn huyu membe mnafiki sana kwanini usubiri mpaka mtu amekufa ndio useme jambo kama hili?
Si angesema tu kipindi kile kile watu wajue ubaya wa jpm. Sasahivi ndio anajifanya kuanika mabaya aliyofanyiwa, Bogus kabisa HUYU Jamaa.
 
Ni wachache wataelewa jinsi alivyo ikoroga hiyo pointi uliyoandika ya Mwisho mkuu, mi nimekuelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…