Uchaguzi 2020 Membe anaweza kutuvusha upinzani kuliko Lissu

Uchaguzi 2020 Membe anaweza kutuvusha upinzani kuliko Lissu

Countrywide

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2015
Posts
20,694
Reaction score
32,527
Nimefuatilia na kumsikiliza kwa makini sana Mh. Membe (jasusi mbobezi) na nimekubaliana nae kuwa anaweza kuwa mtu sahihi sana kuliko wagombea wengine wa upinzani.

Membe ana uwezo wa kujenga hoja na ikakubalika hii ni kutokana na ujasusi wake hivyo ni faida kubwa sana kwa Upinzani
Membe ana utumishi uliotukuka ukilinganisha na wagombea wengine wa upinzani, hivyo kuna faida nyingi kuwa mgombea wetu wa upinzani.

Membe ni mwanadiplomasia nguli na anaweza kuirudisha Tanzania mahali ilipokuwa kimataifa.

Membe ni karata turufu sana kwa wakati huu kwa kuwa ameshajimbambanua kupambana na Magu, hivyo ameshajiandaa na urais.

Upinzani tumpe nafasi membe apeperushe bendera yetu kuliko kuwaachia wengine ambao sidhani kama wana ushawishi kama Membe

#2020upinzani na jasusi mbobezi#
 
Kumbe huwa hamjifunzi tu? Why msirecruit wanachama wenu ambao mmetoka nao mbali na die hard fans wa vyama vyenu? Kwa kufuata huu upepo na gesi ya Pepsi,CCM itaiongoza nchi hii kwa miaka mingine 30 au 50 ijayo
 
Wanachama wetu wapo vizuri na wanaweza ila kwa mwaka huu wacha twende na Membe jasusi mbobezi, huyu ni dawa kwa ccm
Kumbe huwa hamjifunzi tu? Why msirecruit wanachama wenu ambao mmetoka nao mbali na die hard fans wa vyama vyenu? Kwa kufuata huu upepo na gesi ya Pepsi,CCM itaiongoza nchi hii kwa miaka mingine 30 au 50 ijayo
 
Nimefuatilia na kumsikiliza kwa makini sana Mh.Membe(jasusi mbobezi) na nimekubaliana nae kuwa anaweza kuwa mtu sahihi sana kuliko wagombea wengine wa upinzani.
Membe ana uwezo wa kujenga hoja na ikakubalika hii ni kutokana na ujasusi wake hivyo ni faida kubwa sana kwa upinzani
Membe ana utumishi uliotukuka ukilinganisha na wagombea wengine wa upinzani, hivyo kuna faida nyingi kuwa mgombea wetu wa upinzani.
Membe ni mwanadiplomasia nguli na anaweza kuirudisha Tanzania mahali ilipokuwa kimataifa.
Membe ni karata turufu sana kwa wakati huu kwa kuwa ameshajimbambanua kupambana na Magu, hivyo ameshajiandaa na uraisi.
Upinzani tumpe nafasi membe apeperushe bendera yetu kuliko kuwaachia wengine ambao sidhani kama wana ushawishi kama Membe
#2020upinzani na jasusi mbobezi#

Hapo ndio unaona umetuchota mawazo na akili zako za kiccm! Hata kama umeleta huu uzi kwa kejeli, kwanini usimkejeli huyo Membe aanzishe chama chake ili huo ubobezi wake uonekane? Au yeye ubobezi wake unaweza kuonekana kwenye vyama vya wanaume wenzake tu?
 
Huyu Membe akigundua hawa janja janja CCM wameiba kura sidhani kama atakubali usuluhishi kama alivyofanya lowassa...

Upinzani jaribuni kete yenu kwa Membe huwenda akawatoa kimasomaso...
 
Watu wanaweka nguzu nyingi kwenye wasifu wa mtu binafsi kuliko sera za vyama. Bila sera madhubuti na malengo yanayofikika, hata aje malaika hawezi kutuvusha.
 
Back
Top Bottom