Membe be careful, adui yako wa kweli humjui!

Mwaka wa uchaguzi hayo mambo huwa yanatokea na baada ya uchaguzi hautawaona.
Miaka ya 2008 hadi 2014 Viongozi wengi walikuwa wanatumia hii platform ya JF kwaajili ya kuchangia hoja mbalimbali either kupitia Majina yao halisi ama bandia

Ilifikia wakati hoja nzito nzito za akina Kitila Mkumbo ama za akina Tundu Lissu Kwa ID kificho zilikuwa zinapishana kutuhabarisha humu

Wale waliokuwa Jikoni, waliweza kutupatia taarifa ficho kuhusu mengi yaliyokuwa yanatokea Serikalini na Chamani

Ndiyo maana jina la Mgombea wa CCM wa Mwaka 2015 lililetwa humu Mwaka 2014

Anyways, Wakati si milele
 
Issue sio hivyo mazingira ya kisiasa yanabadilika mkuu .

Kwa sasa kuna mambo unabidi kuwa mtazamaji tu.
 
Na kwa sasa wimbi la wasomi wa namna hii linazidi kuongezeka kiasi cha kwamba wakongee wanabaki wanajiuliza hii nchi miaka ya mbeleni itakuwaje
 
Mwenye JF mwenyewe kachangia hii forum kuharibika. Sasa ni mamluki kibao wa kulipwa ndio wapo humu.
Lakini pia tabia za kuanzisha mahusiano ama kupenda kuchat PM

Vijana wengi hawana vifua, mnaweza kuwasiliana huko PM baada ya muda unakuta habari zako zipo Kwa members wengine humu

Unakuta wamedukua hadi picha zako halisi na kutumiana 🙌
 
Jina lililetwa na Bwana Mayalla i think so
 
Wakati sio milele , JF imepoteza misingi yake kwa sasa kimekuwa kijiwe cha matusi , kejeli n.k

Nafikiri na umri wawatumiaji wa zamani ulichangia kuibua na kuleta hoja fikirishi.
 
And now.....🥲🥲🥲
Kipindi hiko jf ni jf kweli sio sshv upuuzi mtupu

Kipindi hiki Uzi unaletwa usiku baada ya siku mambo yatatokea🙌
But now duh
 
Wakati sio milele , JF imepoteza misingi yake kwa sasa kimekuwa kijiwe cha matusi , kejeli n.k

Nafikiri na umri wawatumiaji wa zamani ulichangia kuibua na kuleta hoja fikirishi.
Sahihi Mkuu

Wengi tayari walikuwa kwenye Ofisi kubwa kubwa kuliko ilivyo sasa

Ambapo Vijana wengi humu bado wanatembea na bahasha ama bado ni ma- juniour huko makazini

Kwahiyo hawapati classified info
 
Issue sio hivyo mazingira ya kisiasa yanabadilika mkuu .

Kwa sasa kuna mambo unabidi kuwa mtazamaji tu.
Kisomi haiko hivyo... Sasa kama chuoni ilitegemewa ufundishwe mantiki ili iweje?

Msomi anapoona kuwa anatakiwa awe mtazamaji, wajibu wake (Role) kama msomi kwa jamii ni upi? Jee jamii ikiongozwa na wasiosoma wananchi wawalaumu wasomi kwa kuwa watazamaji au wasiosoma kwa kujaribu kutafuta ufumbuzi kwa matatizo yanayoikabili jamii?
 
Na kwa sasa wimbi la wasomi wa namna hii linazidi kuongezeka kiasi cha kwamba wakongee wanabaki wanajiuliza hii nchi miaka ya mbeleni itakuwaje
Nilikuwa mahali mwanafunzi mmoja wa shahada ya uzamili (Masters degree) akawa anatumia Chatgpt siyo imuongoze kuandika tasnifu (Dissertation) yake, bali alikuwa anaitumia kuandikia hiyo tasnifu yenyewe!!
 
Ni kweli Ila ukiingia katika matatizo atakayeumia ni wewe na familia yako

Hao wakongwe sio wajinga kuzitelekeza I'd zao na kuamua kuwa wasomaji wa habari.
 
KATAA WAHUNI, OKOA TANGANYIKA.✍️📌
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…