Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 57,951
- 32,619
Membe: Serikali haiwezi kurudisha kesi ya Ahmed Ghailani
Sadick Mtulya
SERIKALI imesema, haiwezi kuiomba Marekani ihamishe kesi ya tuhuma za ugaidi inayomkabili raia wa Tanzania nchini humo, Ahmed Ghailani, kuja kuendeshwa nchini.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe aliiambia BBC jana kuwa suala hilo ni gumu kwa kuwa serikali haijawahi kufanya hivyo kwa Mtanzania yeyote.
Alisema serikali ina takwimu ya Watanzania 101 walioko magerezani katika nchi mbalimbali duniani,lakini haijawahi kuziomba nchi husika ili kesi za Watanzania hao, zije kusikilizwa nchini.
Ahmed Ghailani alikamatwa nchini Pakistani mwaka 2004 akihusishwa na ulipuaji mabomu katika majengo ya balozi za Marekani nchini Tanzania na Kenya mwaka 1998, kupelekwa katika kambi ya Guantanamo.
Anatarajiwa kufikishwa katika mahakama ya kirai ya jijini Newyork, Marekani siku yoyote kuanzia sasa kujibu mashtaka hayo.
"Litakuwa jambo gumu kwa serikali kuomba mashtaka yanayomkabili Ghailani, yaje kuendeshwa nchini kwenye mahakama zetu kwa kuwa hatujawahi kufanya hivyo kwa Mtanzania yeyote," alisema waziri Membe.
Kwa mujibu wa Waziri Membe, Tanzania inachoweza kufanya ni kuwasaidia Watanzania walioko magerezani, msaada wa kisheria kabla na baada ya kuhukumiwa.
"Nchi yetu inaheshimu sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa na nchi husika, na tunachoweza kufanya ni kumsaidia Ghailani na watanzania wengine waliokamatwa, kwa kuwapa msaada wa kisheria kama watakuwa wamekwisha hukumiwa au bado," alisema Membe.