Memories! Once upon a time there was Nokia

Bigmaaan

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2023
Posts
306
Reaction score
699
I love tech. Phones are part of it.

Leo nilikutana na fundi simu mmoja wa miaka mingi sana. Nakumbuka mwaka 2009, kabla Simu za laini mbili hazijakuwepo, huyu fundi alikuwa anakata laini na kuziunga kisha ukiweka kwenye simu, inakupa uwezo wa kuswitch from SIM 1 to 2 at your selection. Sijui ilikuwa teknolojia gani ile, ila ilisaidia sana utunzaji na utumiaji wa laini. Sikumbuki alikuwa akicharge bei gani. But then nilikua ninatumia Nokia 6 Buttons.

Teknolojia imetoka mbali sana. Wakati huo Nokia ndio ilikuwa Habari. Wale jamaa walitengeneza simu zenye 'body' imara sana. Battery ilikuwa safi kabisa.

Bahati mbaya teknolojia ukifanya mistake, wenzako wanalitumia na kukupiga gap. Kosa la Nokia kutoingia Android mapema to me ndio 'what broke the camels back'.

Mwaka 2014 nilinunua Nokia Lumia. Ikitumia OS ya Window. Ilikuwa ya kipumbavu kwa namna nyingi. WhatsApp ilikusa limited na features nyingi. Apps nyingi ambazo wadau wangu waliokuwa na Blackberry na HTC walikuwa wana enjoy sana. Bahati nilivunja kioo, sikuwahi kipata hadi leo simu ile iko store.





 
Windows phone OS ambayo ilinunua nokia wangekomaa kidogo ingetoboa basi tu waliamua kuiua mapema.
Kusema kweli android ya kipindi kile ilikuwa takataka isipokuwa ilikuwa open kwa muundani yeyote kuitumia basi developers wengi wakaona ndiko ela ilipo kuunda apps zao.
Ila ilikuwa ima crash crash sana.
Mimi android ya kwanza kuitumia ilikuwa 2010 ama 2011 na nilipewa sikuwa na ubavu wa kuinunha. Ilikuwa ni htc ile ilikuwa unaipush katikari display inainuka inaacha keyboard wazi. Nadhami ni htc g2.
Sema ilikuwa ina drain battery vibaya kabsa.
 
 
Pia Microsoft alichelewa kuingia kwenye game ya OS ya simu. Alikuwakuta tayari Android wameshapendwa sana na App Developers.

CEO wa Huawei, Ren Zhenfei alisema teknolojia ya simu inabadilika kwa kasi sana, na yeye sera yake decision makers ni Tech Engineers na sio 'Briefcase guys'.
 
Nokia kaitoa windows phone from scratch mpaka Sept 2013 ambayo Nokia aliuza device division to Microsoft mauzo yalikua ni 10M units kwa Robo mwaka. Microsoft mwenyewe ndio akaja kuharibu wakati huo Nokia hayupo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…