Meneja Mradi SGR: Treni ya umeme haitatumia umeme huu unaokatika mara kwa mara, inajengewa mtandao wa umeme unaojitegemea

Meneja Mradi SGR: Treni ya umeme haitatumia umeme huu unaokatika mara kwa mara, inajengewa mtandao wa umeme unaojitegemea

mshale21

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
2,126
Reaction score
5,068
Meneja Mradi wa Treni ya SGR Mhandisi Machibya Masanja, amesema kuwa Treni ya umeme itakapoanza haitatumia umeme huu wa kawaida unaokatika mara kwa mara, bali inajengewa mtandao wa umeme unaojitegemea.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Novemba 30, 2021, wakati wa mahojiano maalum na East Africa TV, na kusema kwamba hadi sasa serikali imeshatumia si chini ya bilioni 71 kwa ajili ya ujenzi wa mtandao huo.

Soma pia: Uzi mkuu unaoonesha yaliyojiri kwenye mradi wa SGR tangu kuanza kwake mpaka mradi ulipofikia hivi sasa

"Sasa hivi tunajenga mtandao wa umeme mahususi kwa ajili ya uendeshaji wa Treni, hautaingiliana na matumizi mengine ili kuondoa risk ya umeme kukatika, na mpaka sasa tumetumia si chini ya bilioni 71 kujenga mtandao huo," amesema Mhandisi Masanja.
 
Wangetumia huu mtandao unaokatika katika ili nao wapate machungu ya hii kero ya kukatika umeme pale umeme utapokatika wakiwa kwenye safari zao kwa hiyo SGR, wanaishi uzunguni umeme haukatiki, maofisini haukatiki, dawa yao ilikuwa ni SGR uwakatikie ili waharakishe kutuondoa kwenye hiyo kero.
 
Huo umeme utatumia nini maji, gesi, upepo au sola? Hawa viongozi wanatu dharau sana aisee
 
Ni ujanja ujanja mtupu.
Kwani tatizo la umeme wa Tz kukatika ovyo tatizo ni mtandao?

Ni vipi huo mtandao hautaathiriwa na mgawo wa umeme?

Kama hospitali na mamlaka za kusambaza maji zinaathiriwa na mgawo wa umeme, ni kipi cha ajabu SGR isihathirike?
 
Umeme utatoka wapi ? Bila ya Bwawa la Nyerere hakuna umeme Tanzania zaidi ya huu tulio nao, labda kama watazalisha umeme wao binafsi, wakitumia umeme wa Majenereta haitowezekana ni bora tu waweke treni za diesel engines .

Magufuli bado hakueleweka, unahitaji IQ kiwango fulani kuelewa mipango ya Magu vinginevyo utabakiza chuki na mipasho tu kama tuonavyo sasa hivi, kulikuwa na sababu ya msingi kuzalisha Umeme kwa nguvu ya maji kwani ni umeme wa bei rahisi kuliko yote, na ni wetu 100% .
 
Meneja Mradi wa Treni ya SGR Mhandisi Machibya Masanja, amesema kuwa Treni ya umeme itakapoanza haitatumia umeme huu wa kawaida unaokatika mara kwa mara, bali inajengewa mtandao wa umeme unaojitegemea.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Novemba 30, 2021, wakati wa mahojiano maalum na East Africa TV, na kusema kwamba hadi sasa serikali imeshatumia si chini ya bilioni 71 kwa ajili ya ujenzi wa mtandao huo.

"Sasa hivi tunajenga mtandao wa umeme mahususi kwa ajili ya uendeshaji wa Treni, hautaingiliana na matumizi mengine ili kuondoa risk ya umeme kukatika, na mpaka sasa tumetumia si chini ya bilioni 71 kujenga mtandao huo," amesema Mhandisi Masanja.
Duh. Huko TRC wamejazwa Wasukuma watupu. Magu aiseee Mungu anakuona
 
Meneja Mradi wa Treni ya SGR Mhandisi Machibya Masanja, amesema kuwa Treni ya umeme itakapoanza haitatumia umeme huu wa kawaida unaokatika mara kwa mara, bali inajengewa mtandao wa umeme unaojitegemea.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Novemba 30, 2021, wakati wa mahojiano maalum na East Africa TV, na kusema kwamba hadi sasa serikali imeshatumia si chini ya bilioni 71 kwa ajili ya ujenzi wa mtandao huo.

"Sasa hivi tunajenga mtandao wa umeme mahususi kwa ajili ya uendeshaji wa Treni, hautaingiliana na matumizi mengine ili kuondoa risk ya umeme kukatika, na mpaka sasa tumetumia si chini ya bilioni 71 kujenga mtandao huo," amesema Mhandisi Masanja.
Asije akaipinga kauli yake wenye nchi wakija na kauli yao.
 
Kwahiyo tusitegemee suluhu ya ya kudumu katika tatizo la umeme.
hapana, suluhu ya kudumu ya umeme ipo

Nyerere Hydropower itatumia vyanzo tofauti vya maji na litakuwa failsafe, halishindwi dhidi ya:

mabadiliko ya tabia nchi
ng'ombe za wasukuma zinazokunywa lita 40 kwa siku
ukaidi wa binadamu wanaochepusha vyanzo vya maji
watendaji waoga wa kuzima umeme na kupitiliza ukarabati wa miundombinu
wakulima wa mabondeni wanaozuia njia za asili

Ndivyo Samia na Makamba walivyotupanga
 
Huo mradi wa SGR hautafanikiwa KABISA kwasabab umejaa dhulma ,wizi, ufisadi na mikono iliyojaa damu. Matrillion yamekopwa na watu wametafuna 10% hela ya wastaafu wameiba. Miradi yote CCM huanzisha si kwa ajili ya wananchi bali ni njia ya upigaji.

#MboweSiyoGaidi

YEHODAYA
Punguza majungu utazeeka vibaya. Be positive hata kwa maslahi ya watoto wako tuu. Chadema in chama cha siasa kinachoweza kubadilishwa au kuungana na ccm kwa maslahi mapana ya taifa. Sio dini hiyo.
 
Wametambika?,mnaweza mkamaliza tu kujenga bwawa na maji yakapungua MTO rufiji.
#Tupowenye maji msione tu yanatiririka Tupo ambao tupo
 
Back
Top Bottom