Meneja TARURA Nyamagana anachukua "Ten percent" kilio barabara Isamilo Mwanza

Meneja TARURA Nyamagana anachukua "Ten percent" kilio barabara Isamilo Mwanza

Nyanswe Nsame

Senior Member
Joined
Jul 9, 2019
Posts
165
Reaction score
181
Meneja TARURA Nyamagana anachukua "Ten percent" kilio barabara Isamilo Mwanza


Hii ni hatari, katika barabara ya Isamilo kata ya Isamilo Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, watembea kwa miguu hawana eneo lao maalumu la kutembelea.

Eneo ambalo limewekwa msitari kwa ajili yao ni finyu na hatari kwa usalama wao.

Eneo hilo, kutokana na kuwa finyu, kanawalazimu watembea kwa mguu kuingia katika njia ya vyombo vya moto.

Ufinyu wa eneo hilo, kunatajwa kumekuwa kukisababisha ajali za mara kwa mara na wakati mwingine watu kupoteza maisha.

Licha ya Isamilo kuwa na Diwani na viongozi wengine ambao wengi wao wanaishi katika kata hiyo lakini hawajawahi kulisemea tatizo hilo.

Pia mkandarasi aliyejenga barabara hii, naona hakujali kabisa watembea kwa mguu, Wala eneo la kupita hata baiskeli.

Hivi meneja wa Tarura mkoa na wataalamu wenzake waliona tatizo hilo au ndio zile tunasikia walipiga na mkandarasi.

Inaelezwa kwamba Meneja wa Tarura mkoa Mwanza ambaye kwa sasa kahamishiwa Dodoma na meneja wa Wilaya ya Nyamagana nasikia walishirikiana kuihujumu barabara hii.

Inaelezwa wawili hao walichukua ten percent kwa mkandarasi wa barabara hiyo na ndio maana haya yote yametokea.

Ten Percent kwa watumishi wengi imekuwa ikileta kilio kwa wananchi ambao ndio wahanga wakubwa.

Pamoja na hilo lakini tatizo hili la barabara, linaonesha ni namna gani wataalamu wetu hususani ni meneja wa TARURA uwezo wao ulivyo mdogo.

Kutokana na hili, tunaomba Mtendaji mkuu wa TARURA nchini, atuondoleee huyu meneja wa TARURA Wilaya ya Nyamagana kama alivyo fanya kwa meneja wa mkoa.

Kama aliweza kumuondoa meneja wa mkoa tunaomba amuondoe na meneja wa Wilaya ya Nyamagana, Mohamed Muanda.

......................................
 

Attachments

  • IMG20200513193942.jpg
    IMG20200513193942.jpg
    59.1 KB · Views: 3
  • VID20200513193944.mp4
    46.2 MB
Sijaona ulipomuunganisha na 10%
 
Back
Top Bottom