Meneja wa CRDB Bukoba na Katibu tawala wapanda kizimbani Bukoba leo.

Meneja wa CRDB Bukoba na Katibu tawala wapanda kizimbani Bukoba leo.

Richard

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2006
Posts
15,692
Reaction score
23,038
Meneja wa benki ya CRDB mkoani Kagera Carlo Sendo na aliekuwa katibu tawala wa mkoa huo bwana Amantus Msole ni miongoni mwa watuhumiwa wanne walofikishwa kwenye makahama ya hakimu mkazi ya Bukoba Dennis Mpelembwa mapema leo asubuhi.

Watuhumiwa hao na wengine bwana Simbaufoo Swai ambae ni mhasibu mkuu wa mkoa wa Kagera na mkurugenzi wa manispaa ya Bukoba bwana Steven Makonda wanatuhumiwa kwa pamoja kushirikiana kufungua akaunti namba 015225617399 kwenye tawi la benki ya CRDB tawi la Bukoba ili kujipatia fedha za michango ya maafa ya waathirika wa tetemeko la ardhi.

Akisoma mashtaka yao mwendesha mashtaka mwandamizi wa serikali mkoani humo bwana Hashim Ngole alisema mnamo tarehe 19 mwezi huu washtakiwa walitenda kosa hilo la kufungua akaunti wakikwepa agizo la waziri mkuu Mheshimiwa Kassim Mjaliwa ambae aliagiza wafungue akaunti maalum ambayo tayari ilifunguliwa akaunti yenye namba 0152225617300 ili kuendela kukusanya michango ya maafa.

Serikali mkoani Kagera ilifungua akaunti yenye jina "Kamati Maafa Kagera" ili kuweka fedha ambazo zinakusanywa kwa ajili ya watu waloathirika na maafa hayo ya tetemeko la ardhi ambalo lilitokea mapema mwezi huu na kusababisha vifo vya watu 17 na kuharibu miundombinu mbalimbali kama barabara, nyumba za makazi na kusababisha watu kukosa mahali pa kuishi.

Sambamba na shtaka hilo pia watuhumiwa wanashtakiwa kwa matumizi mabaya ya ofisi ya umma ambayo ni kinyume na sharia ya kupambana na rushwa sehemu ya 17 ya sheria ya mwaka 2007.

Mamia ya wakazi wa mji ya Bukoba walifurika mahakamani kushuhudia na kuwatambua washtakiwa ambao kama wangefanikiwa walikuwa watoke na fedha ya maana ambazo hawakuzitolea jasho bali ni za michango ya maafa.

Washtakiwa wote wamerudishwa rumande hadi kesho asubuhi na hakimu Mpelembwa ameomba muda apitie mashtaka yote na hawakupewa nafasi ya kukiri au kukataa makosa yao kwa mujibu wa maelekezo ya ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka nchini.

Mapema wiki hii raisi John Magufuli alitengua nafasi za Msole na Makonda kwa tuhuma hizo za ufisadi na wizi wa kalamu, huku waziri mkuu Kassim Majaliwa akimvua madaraka mhasibu mkuu wa mkoa bwana Swai.
 
Picha nataka nimuone bwana Swai , ilo jina la Swai na Pesa dahhhhh
 
Jee walitumia vibaya hio account ? Wamewahi kuweka na kutoa pesa ? Na zilienda wapi...
Janga la Bukoba halija shughulikiwa ipasavyo. Misaada imechelewa sana na mpaka sasa hivi juu ya kuchangwa lakini hali ya misaada ni shida na urasimu.
Watu wana lalamika.
Sasa hawa wakuu ina wezekana nasema inawezekana kabisa walikua na nia ya kusaidia wahanga ambao wana shida.
Na huyu wa crdb kosa lake nini ?
Kama masharti ya kufungua account yametimizwa shida ipo wapi ?
Tusubiri sheria na haki itatamalak
 
Mhasibu mkuu wa mkoa ni ofisi gani?
 
Jee walitumia vibaya hio account ? Wamewahi kuweka na kutoa pesa ? Na zilienda wapi...
Janga la Bukoba halija shughulikiwa ipasavyo. Misaada imechelewa sana na mpaka sasa hivi juu ya kuchangwa lakini hali ya misaada ni shida na urasimu.
Watu wana lalamika.
Sasa hawa wakuu ina wezekana nasema inawezekana kabisa walikua na nia ya kusaidia wahanga ambao wana shida.
Na huyu wa crdb kosa lake nini ?
Kama masharti ya kufungua account yametimizwa shida ipo wapi ?
Tusubiri sheria na haki itatamalak

MAAFA3.jpg


Mkuu, MAELEZO walitoa taarifa kuhusu akaunti hii na ambayo ndiyo ilifunguliwa baada ya ile ya serikali ambayo iliagizwa ifunguliwe na waziri mkuu Kassim Majaliwa.

Ukiangalia namba za akaunti hii hapo juu utaona kwamba zinatofautiana na akaunti inayotuhumiwa kufunguliwa kinyemela.

Tusubiri kesi kamili.
 
Back
Top Bottom