Meneja wa Golikipa Aishi Manula amesema, Djigui Diarra ni usajili bora zaidi wa Yanga katika mafanikio yao ya kutwaa Ubingwa wa ligi kuu misimu (3) mfululizo"
Jemedari Said amesema hajawahi kuona golikipa bora aliyekamilika katika sanaa ya uchezaji kama Djigui Diarra Tanzania katika misimu (10) iliyopita, amemzidi hadi mteja wake Aishi Manula yule wa 2018+ aliyekuwa bora.
"katika kipindi cha miaka 10 sijawahi kuona golie mwenye uwezo kama Djigui Diarra unapaswa kuwa mkweli kwenye jambo linalotaka ukweli. Diarra amekuwa bora mbele ya Manula na magolikipa wote. Ni golikipa bora wa muda wote kwa wachezaji wa kigeni.. Watu wajue nikisema hiki sicho sio kwa sababu nachukia bali namanisha."
Matampi mzuri sana ila footwork yake sio nzuri ukilinganisha na Diara na pia amekuwa na bahati
Dhidi ya Yanga 2 ziligonga nguzo akiwa kasimama ila ni mzuri
Unajua maana ya neno "golikipa bora wa muda wote"?,kacheza Tanzania misimu mingapi? umewahi kuwaona akina Mohammed Mwameja, Omar Mahadhi na Athuman Mambosasa?