OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Mtu anapofanya kazi vizuri apongezwe, mtu anapokosea akosolewe na kushauriwa.
Mimi na wenzangu tunampongeza Meneja Ahmed Ally na wenzake. Kwa kweli wanafanya kazi nzuri, wanatendea haki mishahara na upenzi wao kwa Simba SC. Hawa wana Simba wameirudisha Simba SC kwa mashabiki. Kina Ahmed wanatambua mchango wa wanazi wa Simba, kina Simba Ulaya, Aggy Simba, Mwakitalima, Big, Key Mziwanda n.k.
Kazi wanayofanya kuhamasisha watu wakajaze uwanja imenigusa sana. Wenzetu waliikejeli, lakini Ahmed na wenzake wakapuuza na kusonga mbele. Hatimaye imezaa matunda.
Ahmed na wenzako hamna baya, mnaenda kuacha historia ndani ya klabu yetu. Kwenye stori ya mafanikio ya Simba kutasoma majina ya Ahmed Ally, Rabby Hume, Babu Chacharito n.k.
My Take
Mlioko Dar na mikoa ya jirani zimeni TV nendeni kwa Mkapa.