Meneja wa Simba Ahmed Ally hatukudai, huna baya

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Your browser is not able to display this video.





Mtu anapofanya kazi vizuri apongezwe, mtu anapokosea akosolewe na kushauriwa.

Mimi na wenzangu tunampongeza Meneja Ahmed Ally na wenzake. Kwa kweli wanafanya kazi nzuri, wanatendea haki mishahara na upenzi wao kwa Simba SC. Hawa wana Simba wameirudisha Simba SC kwa mashabiki. Kina Ahmed wanatambua mchango wa wanazi wa Simba, kina Simba Ulaya, Aggy Simba, Mwakitalima, Big, Key Mziwanda n.k.

Kazi wanayofanya kuhamasisha watu wakajaze uwanja imenigusa sana. Wenzetu waliikejeli, lakini Ahmed na wenzake wakapuuza na kusonga mbele. Hatimaye imezaa matunda.

Ahmed na wenzako hamna baya, mnaenda kuacha historia ndani ya klabu yetu. Kwenye stori ya mafanikio ya Simba kutasoma majina ya Ahmed Ally, Rabby Hume, Babu Chacharito n.k.

My Take
Mlioko Dar na mikoa ya jirani zimeni TV nendeni kwa Mkapa.
 
Bila kumsahau pasi 1000 jamaa flani mzaramu mzaramu anaongea balaaaa hasa akishashiba ubwabwa utamsikia simba leo wamepiga pasi chache sanaaa kama pasi laki nane hivii hapo sura kaiweka kihuzuni huzuni kweli πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Bila kumsahau pasi 1000 jamaa flani mzaramu mzaramu anaongea balaaaa hasa akishashiba ubwabwa utamsikia simba leo wamepiga pasi chache sanaaa kama pasi laki nane hivii hapo sura kaiweka kihuzuni huzuni kweli πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Anaitwa aka Simba Ulaya aka Pasi milioni
 
Atuna deni nae,kwakweli siku zinavyozidi kwenda Ahmed Ally anazidi ku-improove anaiva,anafanya kazi za kiwango kikubwa.speech zake zinavutia hana mihemko atukani wala kubughudhi waandishi wa habari.
semaji la CAF[emoji123]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…