Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,509
- 3,756
Wakati meneja wa Tanroads mkoani Morogoro, Godfrey Andalwisye akiondolewa kwa madai ya kutokagua miundombinu, mtendaji mkuu wa taasisi hiyo, Patrick Mfugale amesema barabara ya Morogoro-Dodoma ni chakavu kwa kuwa imejengwa muda mrefu.
Kauli hiyo ya Mfugale imekuja siku moja baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuagiza Andalwisye arudishwe makao makuu kutokana na kutokagua barabara hiyo ambayo daraja lake la Kiyegeya lililoko wilayani Kilosa lilisombwa na maji.
Waziri Mkuu, ambaye juzi alikuwa ameenda eneo hilo kushuhudia ujenzi wa daraja hilo, alishangaa kuona mkoa wenye wahandisi 12, kushindwa kufanya ukaguzi wa barabara na madaraja.
Lakini jana, Mfugale alisema barabara hiyo ilijengwa miaka 40 iliyopita na hivyo imeshatumika muda mrefu ndio maana kila mara wamekuwa wakiifanyia ukarabati.
Alisema kukatika kwa daraja hilo ni jambo la kawaida kiutaalamu kwa kuwa uhai wa makalavati yanayowekwa si zaidi ya miaka 25.
Alisema tayari Serikali iko katika mchakato wa kuijenga upya barabara hiyo na madaraja yake.