Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,925
MWENYEKITI Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, amesema kuwa wajasiriamali wanapaswa kuwa na wazo la biashara kabla ya kukopa fedha.
Alisema hali hiyo huwafanya wajasiriamali hao kushindwa kuendelea kutokana na kukosa elimu ya ujasiriamali.
Mengi alitoa kauli hiyo jana alipotembelea kampuni ya Mr. Oil Skuvi 141 Ltd, iliyoko Kawe jijini Dar es Salaam ambapo pia alizindua tovuti ya kampuni hiyo.
Tatizo la wajasiriamali wengi ni elimu ya biashara. Wengi wanasaka pesa kwanza kabla ya kuwa na wazo la biashara. Ukiwa na pesa, ukakosa wazo la matumizi, pesa hizo zitatafuta matumizi zenyewe. Hapo utaona zinaishia kwenye bia na mambo mengine kwa sababu hukuwa na wazo la jinsi ya kuzitumia, alisema.
Source: Tanzania daima
Mengi alitaja sababu nyingine kuwa ni ubunifu ambapo alisema kuwa wengi hawana ubunifu na ndio maana wanashindwa kuendelea. Kadhalika, Mengi ameiomba serikali kutenga sehemu ya eneo la Tanganyika Packers Kawe, kuwa la viwanda vidogo ili kuwawezesha wabunifu wadogo kuendeleza ujuzi wao.
Kampuni hiyo ambayo ilianzishwa mwaka 1995, inatengeneza vitu mbalimbali kwa kutumia vyumba kama samani yakiwemo madawati, meza, vitanda, mageti pamoja na kunyoosha magari. Kuhusu kudhibiti mapato, alisema, Watu wengi hawajui ni wakati gani wa kudhibiti biashara, wanajibana wakati mapato yanaposhuka lakini wakati mzuri wa kudhibiti biashara ni wakati pato linapokuwa zuri, mapato yakiwa juu ukaweza kudhibiti biashara hata ikiyumba hautatetereka.
Ningeomba mdhibiti matumizi wakati biashara inapaa, alisema.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mr. Oil (141) Ltd, Laibai Kallaghe, alisema lengo la kuanzisha kampuni hiyo ni kuhamasisha vijana kujiajiri wenyewe kwa kuanzisha miradi na biashara mbalimbali.
Kallaghe alifafanua kwamba kampuni hiyo imekuwa ikiwafundisha vijana kazi za ufundi, elimu ya ujasiriamali, elimu ya biashara, utunzaji wa kumbukumbu, upangaji wa bei na utafutaji wa masoko.