The Farmer
JF-Expert Member
- Jan 7, 2009
- 1,658
- 559
Hapo ndipo anapokosea.JK hawezi kuwa inspiration ya mapambano dhidi ya ufisadi.Instead,yeye ni sehemu muhimu ya ustawi wa mafisadi.
Tena mtego mmoja mbaya sana !!!Nina uhakika mkubwa kabisa Mengi anajua anachokifanya..Kwa nionavyo Mengi ana maana kubwa sana kumtaja JK,inawezekana amemtega.
Kwa kifupi ni kuwa Mengi nae ni FISADI ndio maana anapewa nguvu na JK ambaye anaendesha serikali ya KIFISADI.
Hapo ndipo anapokosea.JK hawezi kuwa inspiration ya mapambano dhidi ya ufisadi.Instead,yeye ni sehemu muhimu ya ustawi wa mafisadi.
kama ni hivyo basi ina maana kila mtanzania ni fisadi.
Tuongee ukweli jamani japo sina uhakika Mengi ametoa fedha nyingi kupeleka watoto India kutibiwa moyo. Je Rostam aziz mbali ya kumpa hela Mtikila ni lipi amefanya japo kuonyesha kwamba kile alicho tuibia anarudisha angalau 0.001%.
Mengi ni mfanya biashara aliye huru lakini Rost-tam Aziza ni mwizi, tapeli, jambazi, muua albino, n.k.
Mwenye mapenzi akiona PENGO uita MWANYA......
Hilo ni kanyaboya. Huyu mzee anamtumia JK kama ngao lakini hamaanishi. Kwani huwezi kuwa umezungukwa na mafisadi mpaka kwenye familia harafu wewe usiwe. Unaweza usiwe lakini ukafaidika na matunda ya ufisadi. Hivyo huyu mzee anamtumia kama shield ili asema na jamaa waufyate.
JK kama anadhani kuwa nyota yake inang'ang'aa kachemsha kwa sababu anatumiwa tu.
Hapo ndipo anapokosea.JK hawezi kuwa inspiration ya mapambano dhidi ya ufisadi.Instead,yeye ni sehemu muhimu ya ustawi wa mafisadi.
Waberoya,
Mimi ni miongoni mwa wale tuliokatishwa tamaa na serikali kutumia kodi zetu kuwaandalia makao ya hadhi pale Keko wale wezi. Tangu hapo, sioni ni kitu gani kitanishawishi kuwa serikali hii kweli ina dhamira yakupambana na ufisadi. Ni usanii tu!
Lakini hili la Mengi kuua vyama vya siasa, unaweza kutusaidia tulio gizani?
Mengi is so smart, wait you will see! taratiiiiiibu mpaka kitaeleweka.
.....i second you on the bolded part,na kwa taarifa tu ni kuwa RM anamawasiliano 24/7 na JK.Mengi is so smart, wait you will see! taratiiiiiibu mpaka kitaeleweka.
Juzi mbagala angalau Manji kajitutumu, RA sijasikia kapeleka.
RA yeye anafadhili CCM tena kwa hela nyingi na pia nina hakika Igunga atakuwa kapiga tafu sana!
Katika taarifa ya habari ya juzi usiku, Mzee Mengi aliwataja watu watatu wanaompa ujasiri wa kupambana na ufisadi. Alikuwa akijibu swali juu ya wapi na nani anampa ujasiri. Alimtaja Mwenyezi Mungu, Rais JK na Maskini/wanyonge kuwa ndiyo nguzo za ujasiri wake.
Kati ya nguzo alizotaja nina wasiwasi na ya Rais JK. Lakini jinsi alivyomtega ni vigumu JK kukubali au kukataa hadharani kuwa yeye ni nguzo ya Mzee Mengi.
Eti Wana-JF, mnaonaje kuhusu jibu la Mzee Mengi, JK kweli ni nguzo iliyo upande wa wapinga ufisadi au ni ngao ya adui zetu (mafisadi)?
Anaposema JK anamaanisha Julius Kambarage Nyerere siye huyu aliyefutikwa mifukoni mwa mapapa wa mafisadi.
Ukiangalia wakati anawataja mafisadi tarehe 23 Aprili, utaona jamaa pamoja na kuwa anadai JK anampa kiburi lakini wote aliowataja wana ukaribu kabisa na JK.Mengi is so smart, wait you will see! taratiiiiiibu mpaka kitaeleweka.