Mengi,Bakheresa Kopesheni Wanafunzi wa Elimu ya juu....

zubedayo_mchuzi

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2011
Posts
4,873
Reaction score
1,217
Habari zenu.
Nachukua fursa hii kuwaomba hawa matajiri wawili Tanzania na wengine,wawekeze kwenye elimu hasa kuwakopesha wanafunzi wasiojiweza ili nao waweze kusoma,Ni matumaini yangu wanaweza.
 
Unajua maana ya kuwekeza mpaka useme awekeze kwenye Elimu?, Tutajie kwanza kuna kodi yoyote unamlipa Mengi au Bakhressa? Kama unataka Mkopo kweli nenda benk, kwa bakhressa inapatikana Lambalamba kwa mengi Habari sio Mikopo
 
Je wanafunzi wapo tayari kulipa kwa liba?mfano ukipewa mil 2 unaludisha mil 8 baada ya kumaliza chuo tu kama mpo tayari benk ziingie mkataba na na wanafunzi atakae shindwa kulipa atachukuliwa cheti kwa mujibu wa sheria itakayo tungwa
 
We una matatizo,,hao wanafanya biashara zinazowalipa tu,,hata charity wanazotoa bado wanapewa misamaha ya kodi.
 
Habari zenu.
Nachukua fursa hii kuwaomba hawa matajiri wawili Tanzania na wengine,wawekeze kwenye elimu hasa kuwakopesha wanafunzi wasiojiweza ili nao waweze kusoma,Ni matumaini yangu wanaweza.

Umetumia mbinu kali sana kuitukana Serikali ya Jakaya Mrisho Kikwete.
 
Serikali ambayo inakusanya kodi kwa mengi na bakhresa si iwakopeshe hiyo kodi hao wanafunzi? Yaani mwenye nyumba adai uwakopeshe wanawe ada na yeye anakuna kitambi pembeni! Maajabu ya guiness haya sasa
 
Kama Serikali yenyewe, pamoja na mikono ya chuma iliyo nayo inashindwa kuwa'corner wanafunzi walipe, what do you think of a sole propriator ambaye hana machinery yoyote ?
Tuwaache hao uliowajaja wafanye biashara wanazofanya, maana kwa percentage kubwa ni kama huduma kwa Taifa zima.
 
unajua maana ya kuwekeza mpaka useme awekeze kwenye elimu?, tutajie kwanza kuna kodi yoyote unamlipa mengi au bakhressa? Kama unataka mkopo kweli nenda benk, kwa bakhressa inapatikana lambalamba kwa mengi habari sio mikopo

mbona umekuja mapovu aiseeee
 
Serikali ambayo inakusanya kodi kwa mengi na bakhresa si iwakopeshe hiyo kodi hao wanafunzi? Yaani mwenye nyumba adai uwakopeshe wanawe ada na yeye anakuna kitambi pembeni! Maajabu ya guiness haya sasa

hakuna kinacho shindikanika Dada K
 
Umetumia mbinu kali sana kuitukana Serikali ya Jakaya Mrisho Kikwete.

una nichonganisha na WAZEE wa kutoa kucha....nimewaomba wao wawakopeshe wanafunzi hata kwa kuangalia huitaji wataalamu katika sekta zao then wakimaliza wanarudi kufanya kazi katika viwanda vyao
 
Ni wazo zuri nakuunga mkono...
Mzee Mengi na Bakhresa wawakopeshe wanafunzi wa elimu ya juu!
Wasiishie hapo waikopeshe na wizara ya elimu ili iweze kuwalipa walimu stahili zao!
Waikopeshe wizara ya afya ili mgomo wa madaktari usiwepo tena na waende mbali zaidi kuikopesha serikkali ili iendeshe shughuli zake za kila siku!
 
una nichonganisha na WAZEE wa kutoa kucha....nimewaomba wao wawakopeshe wanafunzi hata kwa kuangalia huitaji wataalamu katika sekta zao then wakimaliza wanarudi kufanya kazi katika viwanda vyao

Hapa sasa nimekuelewa
 
Unachoomba ni kwamba zaidi ya kodi wanazotozwa, matajiri hao waisaidie zaidi serikali!
 
Je wanafunzi wapo tayari kulipa kwa liba?mfano ukipewa mil 2 unaludisha mil 8 baada ya kumaliza chuo tu kama mpo tayari benk ziingie mkataba na na wanafunzi atakae shindwa kulipa atachukuliwa cheti kwa mujibu wa sheria itakayo tungwa

unajua utaratibu wanao tumia BANK OF BARODA KUKOPESHA WANAFUNZI KWA TAWI LAO LA BOTSWANA????
 
mkuu umeenda mbali sana,kwani hawa jamaa hela ambazo huwa wanachangishwa kama kuna ujio wa viongozi wakubwa huwa wanarudishiwa??????
 
Serikali ikishindwa jambo ambalo liko ndani ya uwezo wake jawabu sio jukumu hilo kuwapa raia wengine. Ufumbuzi makini ni kuiondoa madarakani tuu. Baba hawezi shindwa lisha watoto wake halafu eti amlazimishe jirani awalishe wanae.
Chama cha Mapinduzi na serikali yake wameshindwa kuongoza,katika kila sekta ni matatizo tuu. Nenda Afya hali mbaya,Elimu ndio hiyo ni majanga,Utalii unatishiwa na wanyama pori kwisha kwa ujangiri, ulinzi na usalama wa raia na mali zao ndio huo ambao walinzi haohao wanateka,kung'oa meno na kubambika kesi mpaka za mauaji ili raia haohao wanaowalinda wanyongwe. Orodha ni ndefu.
WAONDOLEWE TUU.
 
Kikwete apunguze safari za nje akopeshe wanafunzi. Raha alizoponda Kikwete akiwa Marekani kwa siku 17 huku mama Salma akikodi Private Jet wangeweza kuitumia hiyo fedha kuongeza mikopo ya wanafunzi. Kama serikali hiiya wauza unga na majangili inashindwa kubana matumizi, ni mfanyabiashara mwehu tu ndio atakayejitolea kusaidia inaposhindwa kutimiza wajibu wake
 
Unachoomba ni kwamba zaidi ya kodi wanazotozwa, matajiri hao waisaidie zaidi serikali!

umeisikia kufuru ya Mengi alowaahidi wanafunzi wa shule fulani kuwa atanunua div one kwa mil 200 kama sijakosea....kama div zitakuwa 20...hapo pakoje
 
me MENGI jiran yangu tena nyumba ya 2 toka home kwe2,tamfikishia hiz hbr,mcjar
 
Unajua tatizo sio kukopeshwa tatizo ni kurudisha. Mi nakuunga mkono uliyetoa hoja lakini embu angalia upande wa pili.. Ukishamaliza chuo ukaajiriwa serikalini mengi au bakhresa atakutoa wapi ila umrudishie chake? Kumbuka serikali yenyewe inashindwa kurudishiwa hela zake za mikopo ya wanafunzi hao watu binafsi wataweza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…