Mengi Bwana Abbas alinieleza, na mengi ameingia nayo kaburini hakunambia

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
MENGI BWANA ABBAS ALINIELEZA NA MENGI BALOZI AMEINGIANAYO KABURINI HAKUNAMBIA

Tuko kwenye khitma ya Abbas Sykes Msikiti wa Makuti, Kisiwandui Zanzibar niko bega kwa bega na Sheikh Ibrahim Moeva.

Sheikh Moeva na Abbas Sykes wote wametumikia Tanzania nchi za nje na wakifahamiana vyema.

Nimefahamiana na Sheikh Ibrahim Jeddah mwaka wa 1997 na aliyenijulisha kwake alikuwa Balozi Ramadhani Kitwana Dau siku hizo bado hajawa Balozi.

Basi Sheikh Ibrahim akanambia kuwa jamaa wangependa kusikia wasifu wa Balozi Sykes.

Nimeingiwa na hofu hapo hapo.
Kipi kimenitia hofu?

Nimepata uoga kwa kuwa ikiwa kweli nataka kumweleza Abbas Sykes kwa haki ya kumweleza ni lazima nieleze uhusiano wake au uhusiano wao yeye na kaka zake Abdulwahid na Ally na Zanzibar ndani ya chama cha TANU na ASP wakati wa kupigania uhuru wa Zanzibar miaka ya 1950.

Ninatetemeka.

Ishapigwa fatha na khitma zinakusanywa.

Siwezi kukataa kuzungumza.

Lakini najua unyeti wa historia ya Zanzibar.

Ilikuwa kila ninapolileta suala la Zanzibar katika mazungumzo yangu na Bwana Abbas pale Majlis ghafla atakuwa kimya na ataniangalia na "blank face," kama vile sipo pale mbele yake hanioni.

Ali Mwinyi Tambwe alipata kumfukuza mtu nyumbani kwake kwa kumuuliza habari za Zanzibar.

Kipi kilimghadhibisha Ali Mwinyi Tambwe?

Hamza Aziz tukiwa kwenye Majlis yetu yeye alikuwa akiniambia, "Tafiti Mohamed utajua mimi nimekula kiapo mimi nina miaka 74 sasa watanifunga hawa siwezi jela mimi ''raise some dust."

Kwa maneno mengine Hamza Aziz alikuwa ananiambia kuwa hilo somo ninalotaka kusomeshwa na yeye ni somo gumu sana kwa mwalimu na mwanafunzi pia.

Nikasimama kuzungumza.

Nikaeleza maingiliano ya kidugu yaliyokuwapo baina ya wazee wetu Tanganyika na wenzao Zanzibar kiasi cha Sheikh Hassan bin kuwa katika uongozi wa juu wa TAA na kushiriki katika kuasisi TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Nikaeleza na yaliyopita bila ya kueleza yale yaliyopita yalikuwa kitu gani.

Hapa nikasimama na kuomba dua Allah awasamehe wazee wetu kwa makosa waliyofanya.

Sikuamini masikio yangu.
Msikiti mzima uliitika, "Amin," kwa sauti ya uchangamfu na ya juu.

Hakika historia ya Zanzibar inataka moyo kuieleza.

May be an image of 3 people, people standing and indoor
 
Idu...
Kwa kuwa naandika historia ya Waislam?

Unaponiandikia ukiniita, "Wewe mzee," kidogo inakuwa haipendezi kama nia yako ni kunipa staha kwa ajili ya uzee wangu.

Ikiwa nia ni kuniheshimu basi inapendeza ukiandika, "Mzee Mohamed."
Mzee Mohamed maandiko yako yanatabaisha jinsi ulivyo mdini
 
Idu...
Kwa kuwa naandika historia ya Waislam?

Unaponiandikia ukiniita, "Wewe mzee," kidogo inakuwa haipendezi kama nia yako ni kunipa staha kwa ajili ya uzee wangu.

Ikiwa nia ni kuniheshimu basi inapendeza ukiandika, "Mzee Mohamed."
Achana na jinga hilo..halielewi hata nini ulichoandika, na ni kitu gani ulitaka kuelezea.
Japo mimi nina hamu kuyajua hayo"yaliyopita Zanzibar" kwa undani zaidi. Nini kilitokea hasa hadi ikapelekea kuwa kama ilivyokuwa na ilivyo
 
Idu...
Bahati mbaya kwako ikiwa wewe unaniona hivyo.
Mzee wetu, tunahitaji utupatie historia ya taifa letu bila kuegemea kwenye udini.

Wazee kama wewe walioshuhudia historia ya taifa letu kwa macho yao wamebaki wachache.
 
Unachotakiwa kusema ni ki uongo?
Kama kila kitu cha kweli .. ukweli ni dawa hata kama unauma.
 
Mzee wetu, tunahitaji utupatie historia ya taifa letu bila kuegemea kwenye udini.

Wazee kama wewe walioshuhudia historia ya taifa letu kwa macho yao wamebaki wachache.
Idu...
Haya ninayoandika ndiyo ukweli wa historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Kuacha kuandika ukweli kwa kuogopa Uislam tutapotosha ukweli.

Chuo Cha CCM Kivukoni kwa hofu kama hiyo yako wamejiingiza katika matatizo makubwa kwa kuamini kuwa wanaweza kuwakwepa wazalendo kama Abdulwahid Sykes, Ali Mwinyi Tambwe, Sheikh Hassan bin Ameir kwa kuwataja wachache na wakawa na historia ya TANU.

Kwa hofu kama hiyo yako waandishi wa historia ya Vita Vya Maji Maji walidhani wanaweza kubadili majina ya viongozi wa vita ile na wakabaki na historia ya maana.

Leo tunajua kuwa Songea Mbano jina lake khasa ni Abdulrauf, Mkomanile jina lake ni Khadija.

Binafsi nimepitia historia ya Dockworkers Union (1970) iliyoandikwa na John Iliffe kwa kufanya historia upya kwa kumhoji Islam Barakat aliyekuwa Labour Inspector wa kwanza Mwafrika.

Iliffe kamuhoji Barakat lakini jinsi alivyoeleza historia hii ni tofauti na ukweli niliouona mimi.

Iliffe hakumpa haki yake Secretary General wa Dockworkers Union Abdul Sykes.

Mimi nimekieleza kwa kirefu kisa hiki na washiriki wake wakuu, Mwingereza G. Hamilton, Islam Barakat, Abdul Sykes na Erica Fiah.

Illife alionyesha kuchukizwa na yale niliyoandika alipofanya patio la kitabu changu katika Cambridge Journal of African History.

Prof. Mohamed Bakari amepata kusema kuwa tuandike historia zetu wenyewe kwani tukiandikiwa na wengine wataandika kwa namna sisi hatutapendezewa.

Ndiyo haya leo tuko hapa tunajadili kutafuta ukweli.

Chuo Cha CCM Kivukoni kimeandika historia ya TANU bila ya kusoma nyaraka hata moja ya Sykes.

Nini tafsiri ya jambo hili?
Hawakujua kuwa hao ndiyo waliounda TANU?
 
Idu...
Haya ninayoandika ndiyo ukweli wa historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Kuacha kuandika ukweli kwa kuogopa Uislam tutapotosha ukweli.

Chuo Cha CCM Kivukoni kwa hofu kama hiyo yako wamejiingiza katika matatizo makubwa kwa kuamini kuwa wanaweza kuwakwepa wazalendo kama Abdulwahid Sykes, Ali Mwinyi Tambwe, Sheikh Hassan bin Ameir kwa kuwataja wachache na wakawa na historia ya TANU.

Kwa hofu kama hiyo yako waandishi wa historia ya Vita Vya Maji Maji walidhani wanaweza kubadili majina ya viongozi wa vita ile na wakabaki na historia ya maana.

Leo tunajua kuwa Songea Mbano jina lake khasa ni Abdulrauf, Mkomanile jina lake ni Khadija.

Binafsi nimepitia historia ya Dockworkers Union (1970) iliyoandikwa na John Iliffe kwa kufanya historia upya kwa kumhoji Islam Barakat aliyekuwa Labour Inspector wa kwanza Mwafrika.

Iliffe kamuhoji Barakat lakini jinsi alivyoeleza historia hii ni tofauti na ukweli niliouona mimi.

Iliffe hakumpa haki yake Secretary General wa Dockworkers Union Abdul Sykes.

Mimi nimekieleza kwa kirefu kisa hiki na washiriki wake wakuu, Mwingereza G. Hamilton, Islam Barakat, Abdul Sykes na Erica Fiah.

Illife alionyesha kuchukizwa na yale niliyoandika alipofanya patio la kitabu changu katika Cambridge Journal of African History.

Prof. Mohamed Bakari amepata kusema kuwa turnpike historia zetu wenyewe kwani tukiandikiwa na wengine wataandika kwa namna sisi hatutapendezewa.

Ndiyo haya leo tuko hapa tunajadili kutafuta ukweli.

Chuo Cha CCM Kivukoni kimeandika historia ya TANU bila ya kusoma nyaraka hata moja ya Sykes.

Nini tafsiri ya jambo hili?
Hawakujua kuwa hao ndiyo waliounda TANU?
Kwamba akina Sykes walikuwa waislamu walishiriki kuunda TANU sio sababu ya kudai kuwa waislamu pekee ndio walitoa mchango mkubwa wa kuunda TANU.
 
Ndugunde,
Sijaweza kuelewa vyema unachokusudia.

Screenshot_20210522-142629_Facebook~2.jpg

Labda nikufahamishe historia ya harakati zilivyoanza.

Tanganyika kulikuwa na European Association, Indian Association ila hapakuwa na African Association.

Waafrika wao walikuwa wanawakilishwa na Father Gibbons kutoka MInaki Mission.

Mwaka wa 1929 Kleist akiwa Secretary na Cecil Matoka President wakaasisi African Association.

Haya kayaeleza Kleist katika mswada wa kitabu alioandika kabla ya kufariki kwake mwaka wa 1949.

Katika mswada huo anasema kuwa wasomaji wasishangae kuona waasisi wa AA wengi wao ni Waislam na sababu ni kuwa Kanisa lilikuwa linawakataza waumini wake kujiingiza katika siasa.

Unaweza kusoma haya yote katika: ''Kleist Sykes the Townsman,'' ndani ya kitabu alichohariri John Iliffem ''Modern Tanzanians,'' (1973).

Mwaka wa 1933 Cecil Matola akafariki na nafasi yake ikachukuliwa na Mzee in Sudi.

Sasa ili kuiepusha AA na athari za Uislam katika kushughulikia madhila yaliyokuwa yanawafika Waislam kutoka kwa wakoloni wakaamua kuunda Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika mwaka huo huo wa 1933.

Serikali na Wamishionari walikuwa kitu kimoja wakati wa ukoloni na AA ilikusudiwa kiwe chama cha watu wote.

Ikaonekana Waislam kupambana na ukoloni na wamishionari kupitia AA italeta shida kwa Wakristo waliokuwa ndani ya AA ndiyo ikaundwa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika).

Ndiyo maana wanachama wa mwanzo TANU walitoka Rufiji katika Zawiyya za Tariqa Quadiriyya kiongozi wa Quadiriyya akiwa Mufti Sheikh Hassan bin Ameir.

Hii ndiyo sababu utaona hata dhifa ya kumuaga Nyerere safari ya kwanza UNO 1955 ilifanyika katika Jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.

Mtu aliyetumwa kwenda kutafuta wanachama huko alikuwa Said Chamwenyewe na aliyemtuna alikuwa Abdulwahid Sykes.

Hii ndiyo historia ya TANU.
Hatuwezi kuibadili.

Mzee bin Sudi huyo hapo juu na wake zake watatu.
 
Kwamba akina Sykes walikuwa waislamu walishiriki kuunda TANU sio sababu ya kudai kuwa waislamu pekee ndio walitoa mchango mkubwa wa kuunda TANU.
Lakini jee wewe unaona ndiyo sababu ya kuwaondoa kabisa kwenye historia ya TANU watu kama akina Sykes kwenye nchi hii? Udini ni upande mmoja tu wa pale wanapoelezwa ushiriki wa waislamu kwenye mchakato wa uhuru lakini wanapoondolewa kwenye historia na waandishi wa dini nyingine hiyo ni sawa.

Hamuwachi yakhe!!!!
 
Kuna mahala hapa nchini wametengwa akina Sykes kama watu walioshiriki kuasisi TANU? Au watu wanakataa kuleta hoja kuwa waislamu ndio waliasisi TANU na kuleta uhuru.?
 
MENGI BWANA ABBAS ALINIELEZA NA MENGI BALOZI AMEINGIANAYO KABURINI HAKUNAMBIA

Tuko kwenye khitma ya Abbas Sykes Msikiti wa Makuti, Kisiwandui Zanzibar niko bega kwa bega na Sheikh Ibrahim Moeva.

Sheikh Moeva na Abbas Sykes wote wametumikia Tanzania nchi za nje na wakifahamiana vyema.

Nimefahamiana na Sheikh Ibrahim Jeddah mwaka wa 1997 na aliyenijulisha kwake alikuwa Balozi Ramadhani Kitwana Dau siku hizo bado hajawa Balozi.

Basi Sheikh Ibrahim akanambia kuwa jamaa wangependa kusikia wasifu wa Balozi Sykes.

Nimeingiwa na hofu hapo hapo.
Kipi kimenitia hofu?

Nimepata uoga kwa kuwa ikiwa kweli nataka kumweleza Abbas Sykes kwa haki ya kumweleza ni lazima nieleze uhusiano wake au uhusiano wao yeye na kaka zake Abdulwahid na Ally na Zanzibar ndani ya chama cha TANU na ASP wakati wa kupigania uhuru wa Zanzibar miaka ya 1950.

Ninatetemeka.

Ishapigwa fatha na khitma zinakusanywa.

Siwezi kukataa kuzungumza.
Lakini najua unyeti wa historia ya Zanzibar.

Ilikuwa kila ninapolileta suala la Zanzibar katika mazungumzo yangu na Bwana Abbas pale Majlis ghafla atakuwa kimya na ataniangalia na "blank face," kama vile sipo pale mbele yake hanioni.

Ali Mwinyi Tambwe alipata kumfukuza mtu nyumbani kwake kwa kumuuliza habari za Zanzibar.
Kipi kilimghadhibisha Ali Mwinyi Tambwe?

Hamza Aziz tukiwa kwenye Majlis yetu yeye alikuwa akiniambia, "Tafiti Mohamed utajua mimi nimekula kiapo mimi nina miaka 74 sasa watanifunga hawa siwezi jela mimi ''raise some dust."

Kwa maneno mengine Hamza Aziz alikuwa ananiambia kuwa hilo somo ninalotaka kusomeshwa na yeye ni somo gumu sana kwa mwalimu na mwanafunzi pia.

Nikasimama kuzungumza.

Nikaeleza maingiliano ya kidugu yaliyokuwapo baina ya wazee wetu Tanganyika na wenzao Zanzibar kiasi cha Sheikh Hassan bin kuwa katika uongozi wa juu wa TAA na kushiriki katika kuasisi TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Nikaeleza na yaliyopita bila ya kueleza yale yaliyopita yalikuwa kitu gani.

Hapa nikasimama na kuomba dua Allah awasamehe wazee wetu kwa makosa waliyofanya.

Sikuamini masikio yangu.
Msikiti mzima uliitika, "Amin," kwa sauti ya uchangamfu na ya juu.

Hakika historia ya Zanzibar inataka moyo kuieleza.

May be an image of 3 people, people standing and indoor
BwanaAbbas Na Balozi Abbas watu wawili tofauti?
 
Back
Top Bottom