Mengi: Kwanini nimemuoa K-lynn

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
18,037
Reaction score
33,681


Dk. Reginald Mengi akiwa na Familia yake

Dr. Reginald Mengi alipoulizwa kwanini umemuoa Jackline alijubu hivi: Nimemwoa Jackline kwasababu yuko tofauti na wanawake wengine ambao nimeshawahi kuwa nao.

1. Jackline ananipikia chakula kuanzia chai, lunch mpaka dinner.

2. Jackline ananifulia nguo zangu kwa mikono yake sio mashine

3.Jackline anajua nafasi ya mwanaume na nafasi ya mwanamke kwenye nyumba.

4. Jackline ananipenda ndio mana ananifanyia vitu ambavyo wanaume wengi tunapenda kufanyiwa hasa unyenyekevu wake kwangu.

5. Jackline tofauti na watu wengi wanavyomchukulia hakufuata pesa kwangu bali ana mapenzi ya dhati na mimi.

SOMO LA UJUMBE HUU.
Kama wewe ni mwanamke na umeolewaTafadhali TAFAKARI NA CHUKUA HATUA ZA HARAKA KUIMARISHA NDOA YAKO.

Chanzo: Blogu ya Wananchi
 
Kuna mengi tu huyu mzee hajasema nadhani....Mengi sana....Hadi aanze kufuliwa na kupikiwa si alikuwa keshampenda?
 

Mimi, Hoja Zake Za Msingi Sizioni. Naombeni Msaada Tafadhali!
 
Last edited by a moderator:
Nitofauti na wanawake wengine aliowahi kuwa nao ,du
 
Kwa kauli yake ya kusema yuko tofauti na wanawake wengine aliowahi kuwa nao maana yake amekua anaonja wanawake kama wanavyoonja pombe ya kienyeji kilabuni. Huyu ni lambalamba. Binadamu halinganishwi na mwingine kila mtu ana uzuri wake na ubaya wake bahati mbaya uzuri wa huyu ndiyo ubaya wa yule.

Kwa mtazamo wangu, Mengi anataka ufahari wa kuoa Miss Tanzania na sio ndoa bora, anataka mtu wa kumnyenyekea sio msaidizi kama maandiko yanavyosema na wazi Jakline atanyenyekea (mtaka cha uvunguni sharti ainame). Jackline anataka pesa hakuna mapenzi pale ila mambo mengi yanayotendwa hayasemwi nayanayosemwa hatendwi.
 
Mzinzi tu huyu ndiyo maana analinganisha wanawake. Kwa kauli yake ya kusema yuko tofauti na wanawake wengine aliowahi kuwa nao maana yake amekua anaonja wanawake kama wanavyoonja pombe ya kienyeji kilabuni. Huyu ni lambalamba. Binadamu halinganishwi na mwingine kila mtu ana uzuri wake na ubaya wake bahati mbaya uzuri wa huyu ndiyo ubaya wa yule.
Kwa mtazamo wangu, Mengi anataka ufahari wa kuoa Miss Tanzania na sio ndoa bora, anataka mtu wa kumnyenyekea sio msaidizi kama maandiko yanavyosema na wazi Jakline atanyenyekea (mtaka cha uvunguni sharti ainame). Jackline anataka pesa hakuna mapenzi pale ila mambo mengi yanayotendwa hayasemwi nayanayosemwa hatendwi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…