Yupo sahihi,kuna wanawake wengi ila kumpata mke ni shughuli...sasa kama wanawake aliokuwa nao hata kupika chai hawajui wao wanataka kula hotelini,kwa nini asione raha sasa kupewa alichokuwa anahitaji?
Ndoa siyo kuingia ndani kutwa nzima kushinda na remote huku unachart, wewe ni admin katika magroup kama 10 hivi na kila mada unataka uchangie, akili za kuwaza uchumi huna unachojua wewe ni viwanja vipya kwa ajili ya kutumbua...
Kama akili za kushauri mfungue kitega uchumi kipya huna, ili uonekane una maana yakupasa kufanya hata kazi za ndani ambazo zingefanyika sehemu nyingine kwa gharama na ufanisi mdogo...
Vyovyote utavyosema kuhusu Mengi alichokiosema kuhusu mkewe, UKWELI ni kuwa MWANAUME yeyote haswa katika bara la Africa anahitaji mwanamke anayeweza kumudu kazi zote za ndani,maana yake kama unaweza kunihudumia kwa mikono yako basi upendo wa dhati utajengwa nakukua kati yetu hata kama ulifuata mali..
Wewe endekeza mapenzi ya kwenye tamthilia na roho yako ya gubu,maisha yanasonga unazeeka kabla ya muda nakufa mapema kwa sababu ya msongo wa mawazo...